HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 10, 2019

ATE YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUPATA MREJESHO WA WANACHAMA WAKE

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii



CHAMA cha Waajiri Tanzania (ATE) imeanzisha wiki ya huduma kwa wanachama ili kuwapatia fursa kwa wanachama kutoka sekta mbalimbali kuwapatia mrejesho kuhusiana na huduma zote zinazotolewa na chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Dkt Aggrey Mlimuka amesema Mwezi wa Oktoba ni maalumu kwa wiki ya huduma kwa wateja kimataifa, nao kwa mara ya kwanza wameamua kuanzisha wiki ya mwanachama ili kufahamu kwa undani shughuli mbalimbali zinazofanywa na ATE kwa niaba yao.

Amesema, Wiki hii ya huduma kwa Wanachama imeanza rasmi siku ya Jumatatu ya tarehe 7 Oktoba 2019 na itahitimishwa siku ya Ijumaa ya tarehe 11 Oktoba 2019 ambapo dhamira ya kufanya uwepo wa wiki hii ni
Kutoa fursa kwa wanachama wetu kutupatia mrejesho kuhusiana na huduma zote zinazotolewa na ATE 

Aidha, Mlimuka amesema wiki hii wataitumia kwa Kupokea mapendekezo kutoka kwa wanachama wao ya nini kifanyike au kipi kiboreshwe ili kuifanya ATE kuendelea kuwa Sauti ya Waajiri nchini mwetu.

Mlimuka ameongeza kuwa, watatumia pia kusikiliza na kutoa ushauri kwa wanachama Na rasmi kutakuwa na utaratibu wa kila wiki kutoa Taarifa Muhimu kuhusu masuala ya Sheria za Kazi na Mahusiano sehemu za kazi lengo ni kuwaelimisha waajiri kuhusiana na sheria hizi.

Amesema, dhumuni la kutoa raatifa hizo ni ikiwemo na kuepuka migogoro ya mara kwa mara kwenye maeneo ya kazi na kujenga mahusiano sehemu za kazi mambo ambayo yataleta tija na kuongeza uzalishaji na hatimaye kukuza ustawi wa uchumi wetu. 

Mlimuka ameeleza, taarifa hiyo muhimu itakuwa ikisambazwa kupitia njia mbalimbali za kupeana taarifa kama vile barua pepe (emails), Tovuti ya ATE (website) pamoja na njia nyingine kama mitandao ya kijamii lengo ni kuwafikia wanachama wengi zaidi.

"Napenda kutumia muda huu kupitia vyombo vyenu vya habari kuwashukuru wanachama wote wa ATE waliopo nchi nzima kwa ushirikiano mkubwa ambao wamekuwa wakitupatia katika kutekeleza mambo mbalimbali yaliyo kwenye kalenda ya Chama Chetu," amesema mlimuka.

"Niwaombe tu waweze kutumia wiki hii ya Huduma kwa Wanachama kuwasiliana nasi au kufika kwa wingi moja kwa moja kwenye ofisi zetu za makao makuu zilizopo Mikocheni barabara ya Coca-Cola pamoja na ofisi zetu za kanda zilizopo Rock City Mall Mwanza na AICC Arusha ili wataalamu na watoa huduma wetu waweze kuwahudumia,"

Wiki ya huduma kwa wateja imekuwa ikiadhimishwa mwanzoni mwa mwezi Oktoba kila mwaka.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Nchini (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na chama chao kuanzisha wiki ya mwamachama itakayowawezesha Kupokea mapendekezo kutoka kwa wanachama wao ya nini kifanyike au kipi kiboreshwe ili kuifanya ATE kuendelea kuwa Sauti ya Waajiri nchini mwetu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Nchini (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa chama hicho.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad