Afisa Tarafa wa kata ya Itiso Remidius Emmanuel ameunda timu ya watu sita ya ya siku 21, ili kuwabaini watu wote waliojimilikisha maeneo kinyemela katika kitongoji cha Wali (Kijiji cha Izava) tarafani humo
Afisa Emmanuel, amefikia uamuzi hao baada ya kupokea kero na malalamiko ya wananchi wa tarafa hiyo wanaoonyesha kukerwa na uvamizi wa maeneo ambayo yameendelea kuuzwa na kununuliwa kinyemela na watu kutoka maeneo mbalimbali kufuatia kuwepo kwa madai ya kuuzwa kwa Ekari 100 za kitongoji hicho.
Mapema, afisa Tarafa huyo aliwabana wale wote walioshiriki kuuza eneo hilo, ambao hata hivyo walishindwa kutambua jina la mnunuzi wakidai kwamba walitumwa na uongozi wa kitongoji hicho, Aidha aliyekuwa Mwenyekiti wa kitongoji hicho alipotakiwa kufafanua juu ya jambo hilo, alisema maeneo yaliyouzwa yalikuwa ni ekari tano za wananchi walizopewa na Kitongoji hicho kipindi cha nyuma kauli ambayo wananchi walikataa kumiliki maeneo hayo na kuongeza kuwa madai ya umiliki huo ni hewa.
"Nimeelezwa wapo watu wanamiliki Ekari 100 hadi 200 na zaidi, hatuna tatizo na watu kumiliki maeneo, lakini umiliki huo lazima uwe halali, kama kuna watu walifanya ujanja ujanja wakashirikiana na viongozi wasio waaminifu wakauza maeneo ya kijiji wayarudishe mapema, katika hili ninaunda timu maalum kuchunguza hili, nawakumbusha kijiji hakina mamlaka ya kugawa zaidi ya Ekari 50 na ugawaji huo lazima uzingatie taratibu" Alisema Afisa huyo.
Naye Naye Mwenyekiti wa tume hiyo iliyoundwa, Mohamed Kijuu ameahidi kutimiza jukumu hilo kwa uaminifu mkubwa na kumshukuru kiongozi huyo kwa hatua hiyo kubwa.
" Hiki kinachofanywa na Afisa Tarafa ndio mwelekeo wa Serikali ya awamu ya tano kutatua kero za wananchi,mimi na wenzangu tuko tayari, na huu utakuwa mwanzo wa kukomesha hali hii" amesema Kijuu.
Pamoja na mambo mengine, timu hiyo maalum imetakiwa kutumia weledi katika kufanikisha zoezi hilo na baada ya kukamilisha kazi hiyo watakabidhi ripoti hiyo kwa afisa Tarafa ambayo itasomwa mbele ya wananchi hao.
Mapema kabla ya mkutano huo Remidius aliambatana na Kamati ya Shule, Mtendaji wa kata na kijiji hicho kukagua ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na kusomewa taarifa ya mapato na matumizi katika ujenzi huo wa shule shikizi ya Wali katika hatua ya msingi,Kiongozi huyo ameonya tabia ya baadhi ya viongozi kubadilisha matumizi ya fedha zinazotolewa na wananchi kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Mtendaji wa Kijiji cha Izava Peter Mloli akisoma taarifa ya mapato na matumizi ya Ujenzi wa msingi wa vyumba vitatu katika shule Shikizi ya Wali mbele ya Afisa Tarafa Itiso Remidius Emmanuel(kulia).
Afisa Tarafa Itiso Remidius Emmanuel akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Wali (Kijiji cha Izava ) katika mkutano huo ikiwa ni sehemu ya kutimiza ahadi yake ya kukutana wananchi hao kwa mara nyingine baada ya tarehe 13.10.20 kufika kitongojini hapo na kuikataa taarifa ya Mapato na Matumizi ya Mradi wa Maji baada ya kubaini upungufu mkubwa.
Afisa Tarafa Itiso Remidius Emmanuel akionyesha kuridhishwa na taarifa ya Mradi wa maji Kitongoji cha Wali baada ya kusomwa na mtendaji wa Kijiji cha Izava Peter Mloli (Kulia), Kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya Maji Amos Lugumbau.
Afisa Tarafa Remidius Emmanuel akimhoji aliyekuwa mwenyekiti wa kitongoji cha Wali Julius Mchiwa baada ya kubaini ukiukwaji wa taratibu za kugawa maeneo ya Kitongoji hicho.
Timu maalumu ya watu sita (6) iliyoundwa na Afisa Itiso kwa lengo la kufuatilia na kubaini uhalali wa wale wote walionunua na kujimilikisha maeneo hayo kinyume na taratubu.
Afisa Tarafa Itiso Remidius Emmanuel akionyesha kuridhishwa na taarifa ya Mradi wa maji Kitongoji cha Wali baada ya kusomwa na mtendaji wa Kijiji cha Izava Peter Mloli (Kulia), Kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya Maji Amos Lugumbau.

No comments:
Post a Comment