HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 2, 2019

WAZIRI HASUNGA AWATUNUKU VYETI WAHITIMU WA MAFUNZO YA AGRO STUDIES MJINI JERUSALEM NCHINI ISRAEL

Waziri wa Kilimo nchini Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akimkabidhi Cheti Dayana Novat wakati wa mahafali ya mafunzo ya Kilimo ya Agro Studies yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ICC (Jerusalem International Conventional Center) mjini Jerusalem nchini Israel, leo Tarehe 2 Septemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal,Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo nchini Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akishiriki mahafali ya mafunzo ya Kilimo ya Agro Studies yanayofanyika mjini Jerusalem nchini Israel, leo Tarehe 2 Septemba 2019.
Sehemu ya washiriki wakifuatili mahafali ya mafunzo ya Kilimo ya Agro Studies yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ICC (Jerusalem International Conventional Center) mjini Jerusalem nchini Israel, leo Tarehe 2 Septemba 2019.
Waziri wa Kilimo nchini Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akimkabidhi Cheti Bazil Materu wakati wa mahafali ya mafunzo ya Kilimo ya Agro Studies yanayofanyika (Jerusalem International Conventional Center) mjini Jerusalem nchini Israel, leo Tarehe 2 Septemba 2019.
Waziri wa Kilimo nchini Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na mawaziri, Naibu Mawaziri na Mabalozi kutoka nchi mbalimbali waliohudhuria mahafali ya mafunzo ya Kilimo ya Agro Studies yanayofanyika mjini Jerusalem nchini Israel, leo Tarehe 2 Septemba 2019.

Na Mathias Canal, Jerusalem-Israel

Waziri wa Kilimo nchini Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo Tarehe 2 Septemba 2019 ameshiriki mahafali ya mafunzo ya Kilimo ya Agro Studies yanayofanyika mjini Jerusalem nchini Israel na kuwatunuku vyeti vya kuhitimu wanafunzi 45 kutoka Tanzania.

Katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa ICC (Jerusalem International Conventional Center), Waziri Hasunga amewapongeza vijana hao kwa kuhitimu masomo yao hivyo amewaahidi kuwa serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imejipanga kuboresha mazingira wezeshi kwenye sekta ya kilimo hivyo wanayo nafasi nzuri kuutumia ujuzi walioupata kuboresha kilimo watakaporejea nchini Tanzania.

Mahafali hayo yatajumuisha vijana 1600 kutoka mataifa zaidi ya 12 ambapo kati ya hao vijana 45 ni watanzania, miongoni mwao wanawake wakiwa ni 9 na wanaume ni 36.

Waziri huyo wa kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga amesema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepewa jumla ya nafasi 100 kwa ajili ya kupeleka vijana wa kitanzania kujifunza kilimo cha kisasa nchini Israel hivyo fursa hiyo ni muhimu kwani vijana hao wa Tanzania wamepata ujuzi wanachotakiwa kufanya ni kutumia ujuzi huo kwa manufaa makubwa nchini mwao.

Akizungumza na mtandao wa WazoHuru Blog mara baada ya kuwakabidhi vyeti wahitimu hao Mhe Hasunga amesema kuwa kupatikana kwa nafasi hizo 100 ni kutokana na ombi la Rais wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa serikali ya Israel ili kuwawezesha vijana wengi wa kitanzania kujifunza mbinu na teknolojia za kilimo cha kisasa.

Kadhalika, Waziri Hasunga atakutana na kurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Agro Studies ambapo miongoni mwa mazungumzo muhimu itakuwa ni pamoja na kumuomba uwezekano wa kuongezewa nafasi zaidi ili vijana wengi wa kitanzania waende kujifunza mbinu mpya za kilimo nchini Israel.

Pia, Mhe Hasunga atakutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo nchini Israel kujadiliana nae maeneo mbalimbali na fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta ya kilimo nchini Tanzania.

Katika mkutano mwingine, Mhe Hasunga atakutana na kufanya mazungumzo na wadau wawekezaji wakubwa wa sekta ya kilimo nchini Israel ili kuwaeleza fursa za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania.

Katika ziara hiyo tarehe 4 Septemba 2019 Mhe Hasunga atashiriki mapokezi ya vijana 100 ambao wapo nchini Israel kwa ajili ya kuanza mafunzo yao.

Leo tarehe 2 Septemba 2019 ni siku ya pili ya ziara ya kikazi ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga nchini Israel kati ya siku sita atakazokuwa nchini hapa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad