HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 2, 2019

RADI YAUA NG'OMBE 22 PAPO HAPO MKOANI KIGOMA

Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

NG'OMBE 22 wenye thamani ya shilingi milioni 12 ,wamekufa baada ya Kupigwa na radi iliyoambatana na upepo mkali pamoja na Mvua,katika kijiji cha Kaziramihunda kata ya Gwanumpu wilayani Kakonko mkoani kigoma.

Wakizungumzia tukio hilo wamiliki wa Ng'ombe hizo Abdul Kasungu ,alisema septemba 1 mwaka huu majira ya saa kumi na moja, vijana walikuwa wametoka kuwanywesha maji Ng'ombe katika Kijiji cha msenga ,walipokuwa njiani ulitokea upepo mkali ulioambatana na radi na kuwapiga Ng'ombe 22 ambao walikufa papo hapo.

Alisema kati ya Ng'ombe 20 alizokuwanazo amepoteza Ngombe 16 ambao kila moja alikuwa amuuze kwa shilingi laki sita, alisema wanashukuru kwa kuwa watu waliokuwa wakiwachunga walibaki salama kwa kuwa imetokea ni bahati mbaya hawanabudi ya kulipokea hilo.

Filbert Chibedese alisema yeye Ng'ombe wake sita ndio walikufa wengine walipona,  alisema tukio hilo limewasikitisha kwa kuwa litawarudisha nyuma sana kiuchumi, lakini hawana namna kwa kuwa ni majanga ya kiasili yanayojitokeza bila kutarajia.

Akizungumza na Wananchi hao wakati alipofika katika eneo la tukio Mkuu wa Wilaya ya Kakonko,Kanali Hosea Ndagala alisema tukio hilo ni kama matukio mengine halikutegemea litokee, hivyo watu wanatakiwa kuwa wavumilivu na kutambua kuwa mambo hayo ni mpango wa Mwenyezi Mungu,Kanali Ndagala alitoa pole kwa wote waliokutwa na janga hilo.

" nitoe pole kwa wote mliondokewa na mifugo,ni kweli inaumiza sana na ni hasara kubwa mmeipata, jambo kubwa ni kumshukuru Mungu kwa kuwaponya watu waliokuwa wanawachunga Ng'ombe hao, kikubwa ni uvumilivu msikate tamaa muendelee kupambana haya mambo yanatokea hatuna sababu ya kukata tamaa katika utafutaji poleni sana", alisema Kanali Ndagala.

Aidha aliwataka Wananchi katika kipindi hiki ambacho Mvua zimeanza kunyesha wawe makini na kuepuka kukaa chini ya miti wakati wa radi na Mvua ili kukwepa kupigwa na radi na kusababisha maafa makubwa.
 Mkuu wa Wilaya ya Kakonko,Kanali Hosea Ndagala  akishuhudia NG'OMBE 22 wenye thamani ya shilingi milioni 12  wakiwa wamekufa baada ya Kupigwa na radi iliyoambatana na upepo mkali pamoja na Mvua,katika kijiji cha Kaziramihunda kata ya Gwanumpu wilayani Kakonko mkoani kigoma. 
 Baadhi ya Wananchi wakishuhudia tukio hilo 

  Mkuu wa Wilaya ya Kakonko,Kanali Hosea Ndagala akizungumza na Wananchi kufuatia NG'OMBE 22 wenye thamani ya shilingi milioni 12 kufa baada ya Kupigwa na radi iliyoambatana na upepo mkali pamoja na Mvua,katika kijiji cha Kaziramihunda kata ya Gwanumpu wilayani Kakonko mkoani kigoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad