HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 4, 2019

TFF YAVUNA MILION 500 ZA UDHAMINI KUTOKA BENKI YA KCB

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania, Nd. Cosmas Kimario (kulia), akikabidhi hundi ya shilingi milioni 500 kwa Rais wa TFF,  Wallace Karia, kwa ajili ya udhamini wa Ligi kuu Tanzania Bara. KCB imeendeleza udhamini wa ligi hiyo kwa msimu wa 2019/20 ikiwa msimu wa tatu mfululizo. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania, Nd. Cosmas Kimario (wa tatu kushoto), Pamoja na Rais wa TFF,  Wallace Karia, wakionyesha hundi ya shilingi milioni 500 iliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya udhamini wa Ligi kuu Tanzania Bara. Benki ya KCB imeendeleza udhamini wa ligi hiyo kwa msimu wa 2019/20 ikiwa msimu wa tatu mfululizo. (watatukulia) ni Mwenyekiti wa Bodi Benki ya KCB Tanzania,  John Ulanga, Mkuu wa Idara ya Masoko wa Benki hiyo  Christine Manyeye na Mwanasheria Mkuu waBenki ya KCB Anthonia Kilama, Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa TFF Boniface Wambura na Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao wakiwa katika   hafla ya makabidhiano hayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania, Cosmas Kimario (wa tatu kushoto), Pamoja na Rais wa TFF, Wallace Karia, wakionyesha mkataba wa udhamini wa Ligi kuu Tanzania Bara baada ya kutiliana saini leo jijini Dar es Salaam. Benki ya KCB imeendeleza udhamini wa ligi hiyo kwa msimu wa 2019/20 ikiwa msimu wa tatu mfululizo. (watatukulia) ni Mwenyekiti wa Bodi Benki ya KCB Tanzania, Nd. John Ulanga, wengine ni viongozi kutoka TFF na KCB.
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPBL) Boniface Wambura akizungumza na waandishi wa habari baada ya kusaini mkataba wa udhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bars wenye thamani ya Milion 500 kwa msimu wa mwaka 2019/20.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Benki ya KCB  imengia mkataba na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) thamani ya shilingi za Kitanzania 500,000,000  kwa ajili ya kuwa kabla ya kodi, ulitiwa saini leo.ili kuwa  mdhamini mwenza wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara kwa msimu wa 2019/2020. 

Katika Mkataba huo, TFF watapata  milioni 420 baada ya kukatwa kodi.

Mkataba huo ulitiwa saini  na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB, Cosmas Kimario na Rais wa TFF Wallace Karia leo Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa TFF.\

Kwa mara ya kwanza  KCB lianza kudhamini ligi kuu  msimu wa 2017/18 kwa thamani ya shilingi za Kitanzania 325,000,000 na kuongeza udhamini kwa msimu wa 2018/19 kufikia shilingi za Kitanzania 420,000,000.

 Mafanikio makubwa yaliyopatikana kwa udhamini wa misimu iliyopita ndiyo yameivutia Benki ya KCB kuendeleza udhamini huo kwa kiasi cha shilingi za Kitanzania 420,000,000 kupelekea jumla ya udhamini ndani misimu mitatu kuwa shilingi za Kitanzania 1.165bn.

Hafla ya kutia saini makubaliano hayo imehudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Tanzania, John Ulanga, Katibu Mkuu TFF,  Kidao Wilfred, Mwenyekiti wa bodi ya Ligi Kuu,  Steven Mnguto na Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura, Pamoja na Wakurugenzi wa Bodi na wafanyakazi Benki ya KCB Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kusainiwa mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa  KCB   Cosmas Kimario amesema  kwamba pamoja na dhamira ya benki hiyo kurudisha kwa jamii, udhamini huo pia ni fursa kubwa kwa Benki ya KCB kuwekeza kwenye sekta yenye kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa kukuza ajira na vipaji vya vijana wa Kitanzania.

"Zaidi ya kutengeneza ajira kwenye soka, KCB imewekeza kwenye programu ya KCB 2jiajiri ambayo hadi sasa imetoa mafunzo ya uweledi wa biashara kwa wanawake 256 na vijana 100 kuanzia mwezi Oktoba. “Matarajio ya benki yetu ni kuona Watanzania wengi zaidi wanapata ajira kupitia sekta mbali mbali tunazozigusa.” mesema   Kimario.

“Sisi Benki ya KCB, mbali na biashara tunatimiza wajibu wetu katika jamii inayotuzunguka kwa kuiunga mkono serikali yetu kupinga umasikini nchini. Hivyo pia tunasaidia jamii hitaji kupitia sekta za: elimu, afya, mazingira, wajasiriamali, watoto waishio katika mazingira magumu.” 

Rais wa TFF, Wallace Karia ameishukuru Benki ya KCB  kwa kuidhamini Ligi kuu Tanzania Bara kwa mara nyingine jambo ambalo  itasaidia  kufanikisha baadhi ya changamoto kwenye msimu huu wa ligi kuu 2019/20,  Pia amezitaka  taasisi zingine na watu binafsi kuiga mfano huo kuweza kutoa michango ya hali na mali ili kukuza maendeleo ya soka kwa timu za ligi kuu.

Benki ya KCB ni benki kubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati iliyoanzishwa mwaka 1896 kisiwani Zanzibar. Toka hapo benki imekua na kuenea katika nchi za Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi na Ethiopia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad