HAKUNA RASILIMALI ITAYOPOTEA WALA KUTOROSHWA - DC KYERWA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 10 September 2019

HAKUNA RASILIMALI ITAYOPOTEA WALA KUTOROSHWA - DC KYERWA

Anaandika Abdullatif Yunus - Michuzi TV, Kagera.
Jeshi la Polisi Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera, limefanikiwa kukamata Madini ya Bati Tani 2.152 yenye thamani zaidi ya Shilingi Milioni 46 tayari kusafirishwa Nchi za jirani kwa njia za Magendo.

Akitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Rashid Mwaimu amesema Rasilimali hiyo imekamatwa kwa nyakati tofauti kufuatia taarifa za wananchi wema, walioshirikiana na jeshi la polisi wilayani Kyerwa waliokuwa katika Doria mpakani kwa ajili ya kuhakisha rasilimali za Nchi hazitoroshwi.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya ambae ni Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama Wilaya  amesisitiza kuwa mapambano dhidi ya magendo na wale  wote wanojihusisha na magendo ya aina yoyote ikiwemo Kahawa, Ng'ombe, madini n.k hawatabaki salama na hakuna chochote kitakachopelekwa nje Kupitia Kyerwa.

Kuhusu watuhumiwa na madini yaliyokamatwa Mhe. Mwaimu amesema watuhumiwa watafikishwa mahakamani uchunguzi utakapokamilika, na tayari wamewasiliana na Ofisi ya Madini Mkoa wa Kagera ambapo itahusika kutafuta Soko na mwisho hela itayopatikana itaingizwa katika mapato ya Serikali tayari kupangiwa kazi Nyingine.

Itakumbukwa kuwa Mkuu wa Mkoa Kagera Brig. Jen. Marco Gaguti amekuwa akisisitiza ulinzi wa rasilimali za Nchi hususani Mkoa Kagera, na kuahidi kutoa asilimia za mauzo ya kile kitakachokamatwa kama magendo, kwa kikundi au mtu mmoja atakayetoa ushirikiano au taarifa za kukamatwa kwa magendo husika. Hivyo katika kuongeza motisha Wilaya ya Kyerwa inandaa zawadi kwa waliofanikisha zoezi hilo.
 Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kyerwa ikiendelea kupima uzito wa Madini yaliyokamatwa yakitoroshwa, zoezi lilifonyika katika kituo Kidogo cha Polisi Kagenyi Wilayani humo.
 Jiwe la madini aina ya Bati miongoni mwa madini yaliyokuwa yakitoroshwa ikidaiwa kuwa na ubora wa juu sana.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani Kyerwa Rashid Mwaimu akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya ukamataji Rasilimali madini.
Mifuko iliyofungashwa madini ya Bati yenye zaidi ya Tani 2 baada ya kupimwa uzito huo katika kituo cha Polisi Kagenyi Wilayani Kyerwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad