HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 1 August 2019

MAONESHO YA NANENANE TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA TANZANIA

Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Titus Kamani akijadiliana masuala mbalimbali ya uendelezaji wa Sekta ya Ushirika alipotembelea mabanda katika maonesho ya Nanenane Mkoani Simiyu kulia Bw. Agustino Mbulumi Mkurugenzi wa uendeshaji wa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), kushoto ni Bw. Mombeki Baregu Mkuu wa Kilimo na Huduma za Fedha Vijijini wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT).
Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Simiyu Bw. Ibrahim Kadudu akitoa maelezo kuhusu kazi na majukumu ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania kwa wananchi waliotembelea banda la Tume, pamoja nae ni watumishi wa Tume katika siku ya uzinduzi rasmi wa maonesho ya sikukuu ya wakulima Nanenane kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Afisa Ushirika wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Bw. Boniface Moshi akitoa mafunzo ya masuala ya ushirika katika maonesho ya Nanenane Kitaifa yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad