HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 1 August 2019

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MAONYESHO YA 26 YA NANE NANE MKOANI SIMIYU, AZINDUA MKAKATI WA TAIFA WA USIMAMIZI MAZAO BAADA YA KUVUJA

Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan akionyesha vitabu kuashiria uzinduzi rasmi wa  Mkakati wa Taifa wa Usimamizi wa Mazao baada ya Kuvuna, wakati alipoyafungua rasmi maonyesho ya 26 ya kilimo na mifugo (Nane Nane 2019), katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu.  Kauli mbiu katika Maonyesho ya 26 nane nane 2019 ni "KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KWA UKUAJI WA UCHUMI WA NCHI” Maonyesho haya yanawapa wakulima fursa ya kuonyesha bidhaa zao pamoja na kujifunza mbinu tofauti za kuboresha mazao yao na mifugo kwa ujumla.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, Mkakati wa Taifa wa Usimamizi wa Mazao baada ya Kuvuna, uliozinduliwa leo Agosti 1, 2019 wakati alipoyafungua rasmi maonyesho ya 26 ya kilimo na mifugo (Nane Nane 2019), katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, Mkakati wa Taifa wa Usimamizi wa Mazao baada ya Kuvuna, uliozinduliwa leo Agosti 1, 2019 wakati alipoyafungua rasmi maonyesho ya 26 ya kilimo na mifugo (Nane Nane 2019), katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan akitoa hotuba yake katika ufunguzi rasmi maonyesho ya 26 ya kilimo na mifugo (Nane Nane 2019), katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, akitoa hotuba yake na mpango wa wizara yake katika ufunguzi rasmi maonyesho ya 26 ya kilimo na mifugo (Nane Nane 2019), katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, akitoa hotuba yake katika ufunguzi rasmi maonyesho ya 26 ya kilimo na mifugo (Nane Nane 2019), katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akizungumza katika hafla ya ufunguzi rasmi maonyesho ya 26 ya kilimo na mifugo (Nane Nane 2019), katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza katika hafla ya ufunguzi rasmi maonyesho ya 26 ya kilimo na mifugo (Nane Nane 2019), katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu.
Mbunge wa Jimbo la Bariadi na Mwenyekiti wa Wabunge wa Simiyu, Andrew Chenge akizungumza katika hafla ya ufunguzi rasmi maonyesho ya 26 ya kilimo na mifugo (Nane Nane 2019), katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu.
No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad