HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 8, 2019

Hospitali mpya ya St Monica iliyojengwa na Taasisi ya Kirua Children Care Foundation katika kijiji cha Marua ,kata ya Kirua Vunjo Magharibi katika wilaya ya Moshi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira akiwa ameongozana na Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia pamoja na Mwenyekiti wa Taasisi ya Kirua Children Care Foundation ,Padri Amedeus Macha wakielekea katika ufunguzi rasmi wa Hosptali hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira akitia saini katika kitabu cha wageni alipofika katika Hosptali hiyo kwa ajili ya ufunguzi.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kirua Children Care Foundation ,Padri Amedeus Macha akimueleza jambo mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira wakati akitembelea vyumba vya kulaza wagonjwa katika Hosptali hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira akitizama baadhi ya mashine zilizoko katika Hospitali hiyo.
Chumba cha kulaza wagonjwa.
Padri Amedeus Macha akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira chumba maalumu kwa ajili ya wanawake kujifungulia.
Baadhi ya Vifa vilivyopo maabara ya Hospotli hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira  akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa Hospitali hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira akitoa kitambaa kufungua jengo hilo la Hosptali ya St Monica.
Padri Amedeus Macha akifanya Ibada mara baada ya kufunguliwa rasmi kwa Hospitali hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira akizungumza wakati wa ufunguzi wa Hospitali ya St Monica iliyopo jimbo la Vunjo wilaya ya Moshi.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia hotuba ya Mkuu huyo wa mkoa.
Mbunge wa Jimbo la Vunjo,James Mbatia akizungumza katika hafla ya ufunguzi rasmi wa Hospitali ya St Monica.
Baadhi ya wananchi waliofika katika ufunguzi wa Hospitali hiyo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kirua Children Care Foundation ,Padri ,Amedeus Macha akizungumza katika ufunguzi wa Hosptli hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Kiliamanjaro Dkt Anna Mghwira akiwa katika picha ya pamoja na wageni waliofika kwa ajili ya kushuhudia ufunguzi rasmi wa Hospitali ya St Monica iliyopo kijiji cha Marua ,wilaya ya Moshi .

  Na Dixon Busagaga wa Michuzi TV .

MBUNGE WA Jimbo la Vunjo ,James Mbatia ameshauri kuanzishwa kwa Utalii wa Tiba (Medical Tourism) katika eneo linalozunguka Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) ili kurahisha utoaji wa huduma kwa wageni wanaopata matatizo wakati wa kupanda mlima Kilimanjaro.

Mbatia aliyasema hayo jana wakati wa ufunguzi rasmi wa Hospitali ya St Monica iliyopo jirani na Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro katika kijiji cha Marua ,kata ya Kirua Vunjo Magharibi,katika wilaya ya Moshi  huku akiiomba serikali kusaidia katika uboreshaji wa Miundombinu ya barabara.

Akizungumza  mara baada ya kufungua na  kutembelea maeneo mbalimbali ya Hospitali Hospitali iliyojengwa na Taasisi ya Kirua Children Care Foundation Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira ameipongeza taasisi hiyo kwa kujenga Hosptali hiyo ambayo itasaidia kupunguza changamoto za kiafya kwa wakazi wa maeneo hayo na mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla.

Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya Kirua Children Care Foundation Padri Amedeus Macha amesema Hospitali hiyo itakayo kuwa na uwezo wa vitanda zaidi ya 100 imelenga kutoa huduma za matibabu kwa wazee na watoto ambao  kwa muda mrefu wamekuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za Afya.

Dkt.Bogias Mwamgunda ni mwakilishi wa mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro hapa akaeleza namna ambavyo Hosptali hiyo itasaidia Wazee na watoto katika kupambana na magonjwa yatokanayo na Baridi .
Taasisi za Dini katika jimbo la Vunjo zimekuwa mstari wa mbele katika uwekezaji wa masuala ya huduma za afya ,hali inayochangia urahishaji wa upatikanaji wa matibabu tofauti na ilivyokuwa kwa kutembea umbali mrefu  hasa nyakati za mvua na usiku .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad