Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na
Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, Bw. Alex Mubiru
wakibadilishana hati za mikataba ya mkopo wenye masharti nafuu wa dola
180m, sawa na sh. bilioni 414 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB), kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete (ring road) ama mzunguko
kwa kiwango cha lami umbali wa kilometa 110.2 na uboreshati wa
miundombinu katika Jiji la Dodoma, Makao Makuu ya nchi.

Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia)
akizungumza jambo mbele ya waandishi wa wahabari (hawapo pichani) baada
ya kusaini makubaliano ya mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa dola
180m, sawa na sh. bilioni 414 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB), kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete (ring road) ama mzunguko
kwa kiwango cha lami umbali wa kilometa 110.2 na uboreshati wa
miundombinu katika Jiji la Dodoma, Makao Makuu ya nchi. Kulia kwake ni
Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, Bw. Alex Mubiru.

Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na
Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, Bw. Alex Mubiru
wakitia saini makubaliano ya mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa
dola 180m, sawa na sh. bilioni 414 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB), kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete (ring road) ama mzunguko
kwa kiwango cha lami umbali wa kilometa 110.2 na uboreshati wa
miundombinu katika Jiji la Dodoma, Makao Makuu ya nchi.

Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na
Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, Bw. Alex Mubiru
wakitia saini makubaliano ya mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa
dola 180m, sawa na sh. bilioni 414 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB), kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete (ring road) ama mzunguko
kwa kiwango cha lami umbali wa kilometa 110.2 na uboreshati wa
miundombinu katika Jiji la Dodoma, Makao Makuu ya nchi.

Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na
Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, Bw. Alex Mubiru
wakitia saini makubaliano ya mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa
dola 180m, sawa na sh. bilioni 414 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB), kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete (ring road) ama mzunguko
kwa kiwango cha lami umbali wa kilometa 110.2 na uboreshati wa
miundombinu katika Jiji la Dodoma, Makao Makuu ya nchi.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini-TANROADS, Mhandishi Patrick Mfugale,
akiwaeleza wanahabari kuhusu michoro ya mradi wa ujenzi wa barabara za
mzunguko katika Jiji la Dodoma ambao Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)
umetoa mkopo wenye masharti nafuu wa dola 180m, sawa na sh. bilioni 414
kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa ajili ya kuutekeleza
katika kipindi cha miaka miwili ijayo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia)
walioketi mbele akizungumza jambo mbele ya waandishi wa wahabari (hawapo
pichani) kabla ya kusaini makubaliano ya mikataba miwili ya mikopo
yenye masharti nafuu yenye thamani ya dola 180m, sawa na sh. bilioni 414
kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa ajili ya ujenzi wa
barabara za pete (ring road) ama mzunguko kwa kiwango cha lami umbali wa
kilometa 110.2 na uboreshati wa miundombinu katika Jiji la Dodoma,
Makao Makuu ya nchi. Kulia kwake ni Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo
ya Afrika AfDB, Bw. Alex Mubiru.
Tukio
la kusaini makubaliano ya mikataba miwili ya mikopo yenye masharti
nafuu yenye thamani ya dola 180m, sawa na sh. bilioni 414 kutoka Benki
ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete
(ring road) ama mzunguko kwa kiwango cha lami umbali wa kilometa 110.2
na uboreshati wa miundombinu katika Jiji la Dodoma, Makao Makuu ya nchi,
lililofanyika katika ukumbi wa Hazina Jijini Dar es Salaam.
Kamishna
wa Fedha za Nje Bw. John Rubuga (Kushoto) akiwa na maafisa waandamizi
wa Wakala wa Barabara Nchini-TANROADS, wakifuatilia kwa makini hotuba za
viongozi wa Wizara na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wakati wa
halfa fupi ya kusaini mikataba miwili ya mikopo ya dola milioni 180 kwa
ajili ya ujenzi wa barabara za pete (ring road) ama mzunguko kwa kiwango
cha lami umbali wa kilometa 110.2 na uboreshati wa miundombinu katika
Jiji la Dodoma, Makao Makuu ya nchi, lililofanyika katika ukumbi wa
Hazina Jijini Dar es Salaam.
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
Jiji
la Dodoma na vitongoji vyake, hivi karibuni litabadilika mwonekano wake
na kuwa la viwango vya kimataifa baada ya Benki ya Maendeleo ya Afrika,
AfDB kuipatia Tanzania mikopo yenye masharti nafuu ya dola milioni 180
sawa na shilingi bilioni 414 kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete
(ring road) kwa kiwango cha lami na uboreshaji wa miundombinu katika
Jiji hilo.
Makubaliano
ya mikopo hiyo yametiwa saini Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu
wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, kwa upande wa Serikali,
na Meneja Mkazi wa Benki hiyo hapa nchini, Bw. Alex Mubiru.
Akizungumza
wakati wa hafla ya utiaji saini mikopo hiyo, Bw. Doto James, amefafanua
kuwa mradi utahusisha Ujenzi wa barabara ya mzunguko wa njia nne zenye
urefu wa km 110.2 kwa kiwango cha lami kutoka Nala – Veyula – Ihumwa –
Matumbulu.
Alisema
mikopo hiyo pia inahusisha uboreshaji wa upatikanaji wa miundombinu ya
huduma za kijamii ikiwemo huduma za maji na vituo vya afya; Ukarabati wa
barabara za mchepuko; na Utekelezaji wa mikakati ya usalama wa
barabarani katika mji wa Dodoma itakayotekelezwa katika kipindi cha
miaka miwili” alifafanua Bw. James
”Kupitia
Mikataba hii, Benki ya Maendeleo ya Afrika itatoa kiasi cha dola za
Marekani milioni 138 kupitia dirisha la Benki ya Maendeleo ya Afrika
(ADB Window) na dola za Marekani milioni 42 zitatolewa kupitia mfuko wa
Africa Growing Together Fund (Mfuko wa Serikali ya China unaosimamiwa na
Benki ya Maendeleo ya Afrika)” alisisitiza Bw. James
Aliishukuru
Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za
Serikali za uwekezaji katika miundombinu ya usafiri itakayoiwezesha
Tanzania kufikia azma yake ya kuwa kitovu cha biashara na usafirishaji
katika Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika.
“Uwekaji
saini wa Mikataba hii miwili itaongeza kiasi cha fedha ambacho
kimetengwa na Benki kwa ajili ya miradi ya ujenzi wa barabara nchini
Tanzania, kutoka dola za Marekani milioni 858.16 hadi dola za Marekani
bilioni 1.038, sawa na takribani sh. trilioni 2.39”, aliongeza Bw. James
Alisema
Barabara hiyo inaungana na barabara ya Cape hadi Cairo inayojulikana
kama the Great North Road Highway yenye urefu wa km 10,228 inayopita
katika nchi nane ambazo ni Afrika ya Kusini, Zimbabwe, Zambia, Tanzania,
Kenya, Ethiopia, Sudan na Misri na ni barabara ya ukanda wa kati
(central corridor) inayounganisha Tanzania na nchi jirani za Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Uganda.
Alidokeza
pia kuwa Benki hiyo ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), imeonesha utayari wa
kufadhili ukarabati wa barabara ya Bagamoyo–Pangani-Tanga kwa kiwango
cha lami na Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa-Msalato, utakaojengwa
mkoani Dodoma ambapo tayari maandalizi yameanza.
Kwa
upande wake, Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB), Bw.
Alex Mubiru, alisema kukamilika kwa mradi huo kutaiunganisha Dodoma na
mikoa mingine ikiwemo Arusha, Iringa, Singida, na Dar es salaam na
kwamba utasaidia kupunguza msongamano wa magari katikati ya Jiji la
Dodoma kwa sababu magari yanayokwenda kwenye maeneo hayo yatapita
pembezoni mwa Jiji.
“Benki
ya Maendeleo ya Afrika pamoja na washirika wake tutatoa asilimia 84 ya
gharama za mradi ambazo ni dola za Marekani Milioni 215 wakati Tanzania
itatoa asilimia 16 na baadae mwaka huu tutatoa kiasi kingine cha msaada
wa takriban dola milioni 7.2 ambazo zitatumika kwa ajili ya kuimarisha
mazingira kwa kupanda miti kwenye eneo la mradi” alisema Bw. Mubiru.
Aliongeza
kuwa hivi sasa Benki yake inajiandaa kutoa mkopo kwa ajili ya miradi
miwili muhimu ukiwemo mradi wa uboreshaji wa barabara kutoka
Bagamoyo-Pangani-Tanga-Horohoro/lunga, Lunga – Mombasa-Malindi pamoja na
ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa-Msalato, miradi ambayo Bodi ya
Benki hiyo inatarajia kuipitisha mwishoni mwa mwaka 2019.
Meneja
Mkazi huyo wa AfDB nchini alisema matukio haya yote yanatokea kwa
sababu Benki yake ina imani na kupongeza mafanikio makubwa ya Serikali
ya Tanzania katika kuimarisha maendeleo ya watu wake na kwamba Benki
hiyo iko tayari kuhakikisha azma hiyo inafikiwa.
No comments:
Post a Comment