HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 24, 2019

WATANZANIA UINGEREZA WACHAGUA VIONGOZI WA JUMUIYA - ATUK

Hatimaye Watanzania Uingereza wamewachagua viongozi wa Jumuiya yetu ( Association of Tanzanians UK) yaani ATUK. Juni 2018 mkutano mkuu ulifanyika mjini Reading kufukuzia zoezi hili chini ya ulezi wa Balozi Mheshimiwa Asha Rose Migiro. Mchecheto ulifukuzwa na wengi ila aliyewasha kiberiti alikuwa Joseph Warioba. Baada ya mwaka, siku nzima ya Mtanzania, Jumapili 30 Juni , 2019, ilitayarishwa na wanakamati wa ATUK – ambao baadhi walikuja kuwa viongozi wa Jumuiya. Hapa inaonyesha namna juhudi za Balozi kutuunganisha zilivyoambatanika na ari na hamasa za Watanzania.

Azma kuu ya Jumuiya hii si tu kukutanisha Watanzania kama sauti moja. Pia kuweka ngazi ya kusaidia , kujenga na kuwekeza nyumbani kutokea huku Majuu. Ni jambo la kuchangamkiwa sana. Watanzania toka sehemu mbalimbali za Uingereza walijieleza na kutafuta kura wakipigania nafasi za uenyekiti, katibu na mweka hazina na makaimu wao. Nusu ya kampeni hizi iliendelea mtndao wa WhatsApp na nusu ikakamilika ofisi za ubalozi wetu mtaa wa Bond Street, London, Jumapili 14 Julai, 2019. Uongozi mpya wa ATUK. Waliosimama nyuma. Toka kushoto, Mweka Hazina Msaidizi, Nelson Kampa, (Birmingham); Naibu Katibu, Frank Leo (Coventry), Mweka Hazina, Lucy Shigikile (London). Walioketi, toka kushoto,: Makamu Mwenyekiti, Zuhura Mkwawa (Leicester), Mwenyekiti , Martha Mpangile (London) na Katibu wake, Dk Imani Kondo... Kura ikipigwa ... Sam Mbogo mkazi Wales akijieleza kwa mintaarafu ya kupata kura  Toka kulia, Mwanahabari mkongwe na Mhariri wa The East African, Deo Kamuhanda, akiwa na Simon Mzuwanda (aliyepigania kijasiri wadhifa wa Uenyekiti na kushindwa ), Patricia Mpangala na Joe Wairoba, aliyefanya kazi kubwa kuisimamisha, ATUK.  Ukumbi umejazana Watanzania toka vitengo mbalimbali vya kisayansi, sanaa na akina mama wa TAWA.  Alex Masuguri mmmoja wa wasimamizi wakuu wa shughuli hii muhimu akitangaza matokeo. Wenzake ni kushoto, Batilda Tenga na kulia, Pauline Nzengula.  Mwenyekiti mpya, Martha Mpangile, ( pili kutoka kushoto) na Mweka Hazina , Lucy Shigikile (wa kwanza kulia ) wakipongezwa na kina mama wenzao. Picha na Habari za Freddy Macha 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad