HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 27, 2019

WAZIRI MKUU AVUTIWA NA UWEKEZAJI WA BENKI YA MAENDELEO YA TIB

Na Mwandishi wetu, Dodoma

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amevutiwa na uwekezaji wa unaofanywa na Benki ya Maendeleo ya TIB kwa kuyakopesha makampuni ya wazawa hivyo kuchochea ajira nchini.

Waziri Mkuu alionyeshwa kufurahishwa kwake na bidhaa zilizokuwa zikionyeshwa katika banda la Benki hiyo wakati akitembelea mabanda ya maonesho ya Tamasha la Uwekezaji Dodoma, yanayoendelea jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa kumkaribisha Waziri Mkuu Majaliwa, Mkurugenzi wa Mipango na Mikakati wa Benki hiyo, Bw. Patrick Mongella alisema kuwa Benki ya Maendeleo ya TIB inaendelea kutekeleza kwa vitendo juhudi za serikali kwa kuwezesha uwekezaji wa viwanda nchini ili kuongeza ajira na kuondoa umaskini kwa Watanzania.

“Tumeshiriki Tamasha ili kutangaza fursa zilipo kwenye benki yetu ili kuongeza ufanisi katika kugharamia miradi ya maendeleo ya kiuchumi hasa ile ya kimikakati inayotoa ajira kwa Watanzania,” alisema.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkurugenzi wa Mipango na Mikakati wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Bw. Patrick Mongella (kulia). Kushoto ni Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa benki hiyo, Bw. Joseph Chilambo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiangalia baadhi ya vipeperushi vilivyokuwa vikioneshwa katika Banda la Benki ya Maendeleo ya TIB. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Mipango na Mikakati wa Benki hiyo, Bw. Patrick Mongella (wapili kulia), Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa benki hiyo Bw. Joseph Chilambo (wapili kushoto) na Meneja Masoko na Uhusiano, Bw. Saidi Mkabakuli (kulia).
Mkurugenzi wa Mipango na Mikakati wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Bw. Patrick Mongella (wapili kulia) akimuonesha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto) baadhi ya bidhaa zilizotengenezwa kutokana na mkopo uliotolewa na benki hiyo. Wengine pichani ni Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa benki hiyo Bw. Joseph Chilambo (wapili kushoto) na Meneja Masoko na Uhusiano, Bw. Saidi Mkabakuli (kulia).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad