HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 26, 2019

WADAU WATAKIWA KUJISOMEA ZAIDI ILI KUJIONGEZEA MAARIFA YA MASUALA YA SHERIA

 Na Kulwa Mayombi
Mahakama ya Afrika ya haki za binadamu watu (AfCHPR) yenye makao yake makuu jijini Arusha imewahimiza  wadau mbalimbali kuitumia kikamilifu Maktaba iliyopo katika Mahakama hiyo kwa lengo la kujiongeza maarifa hasa yanayohusu masuala ya sheria.

Alizungumza katika Juma la Maktaba (Library Week) liloratibiwa na AfCHPR. Msajili wa Mahakama hiyo Jaji Sylvain Ore’ alisema kuwepo kwa vitabu vingi,majarida kadhaa na rasilimali nyingine katika Mahakama hayo kunatoa fursa zaidi kwa wadau na wananchi kwa ujumla wa ndani na nje ya nchi kujijengea uwezo wa kujifunza hasa katika masuala ya utetezi na ukuzaji wa haki za binadamu.

“Maktaba na huduma zake ni njia ya kutoa maarifa katika jamii na inatoa nafasi za kujifunza, inasaidia kuboresha mawazo mapya na pia huhakikisha masjala ya kuaminika ya maarifa yaliyopatikana na kukusanywa na vizazi vilivyopita alisema  Jaji Ore’’.”

Kwa mujibu wa Jaji Ore’,AfCHPR imetambua umuhimu huo wa Maktaba hivyo kuiweka moja kwa moja chini ya idara ya usajili tangu ianzishwe Mahakamani hapo mwaka 2009 kwa lengo la kusaidia shughuli za kisheria za  watumishi wa Mahakama,watafiti na wadau mbalimbali.

Alisema kwa sasa Maktaba hiyo katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu ina zaidi ya vitabu 6000 na inatarajiwa vitaongezeka katika kipindi cha Miaka michache ijayo na kuiiomba menejimenti ya Maktaba hiyo kuangalia uwezekano wa kuongeza bajeti ya kununua vitabu zaidi na rasilimali nyingine  za Maktaba ili kuimarisha upatikanaji wa vitabu vya rejea kwa watumiaji wa Maktaba hiyo.

Kwa upande wake Mkutubi wa Maktaba ya Mahakama ya Afrika ya haki za Binadamu na Watu.DR.Fidelis Katonga alisema pamoja na mambo mengine Juma la Maktaba katika Mahakama hiyo  kuonyesha jukumu la Maktaba katika kukuza na  kulinda haki za Binadamu barani Afrika,kuhimiza matumizi ya Maktaba.kupata mrejesho wa watumiaji wa Maktaba hiyo na pia kutafuta Washirika  zaidi wa Maktaba na taasisi nyingine.

Dr.Katonga pia alitaja mafanikio ya Maktaba hiyo tangu kuanzishwa kwake kuwa ni pamoja na kuwa na vitabu Zaidi ya 6000,kuruhusu wadau mbalimbali wakiwemo wananchi kutumia huduma za Maktaba,kuchapisha na kusambaza Nyaraka zinazohusu masuala ya haki za Binadamu na pia shughuli ya AfCHPR.

Alisema upo mpango wa miradi mipya ya Maktaba katika Mahakama hiyo ukiwemo ule wa msingi wa maarifa ya Kiafrica (AKB) utakaohusu takwimu msingi za machapisho kuhusu Afrika na utazileta pamoja Maktaba zote za nchi za Umoja wa Afrika ili kuziweka nyaraka mbalimbali za Afrika katika jukwaa moja na ziweze kupatikana kwa urahisi.

Wadau mbalimbali wamekuwa wakisaidia uimarishaji wa huduma za Maktaba hiyo iliyopo katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu na watu ambao ni Umoja wa Ulaya(EU),Shirika la misaada la Ujerumani(GIZ),Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu,Taasisi ya Raone Walenberg na Maktaba za ndani ya nchi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad