HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 26, 2019

AHAMIAJI HARAMU 12 RAIA WA ETHIOPIA WAKAMATWA MOROGORO

Na Hussein Stambuli, Morogoro
Ofisi ya uhamiaji mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na jeshi la polisi wamewakamata wahamiaji haramu 12 raia wa Ethiopia waliokuwa wamejificha katika pori la kijiji cha Lugono wilayani Mvomero wakitokea Tanga kuelekea mpaka wa Tunduma ili kwenda  nchini Afrika ya Kusini…

Akizungumza na waandishi wa habari afisa uhamiaji mkoa wa Morogoro kamishna msaidizi wa uhamiaji angela shija amesema kukamatwa kwa wahamiaji hao haramu 12 kumetokana na taarifa za kiintelijensia walizozipata juni 24 mwaka huu, ambapo kati ya wahamiaji hao haramu 12 waliomamatwa,tisa walikuwa na pasi za kusafiria ingawa hazikuwa na vibali kwa kuwaruhusu kuingia nchini.

“mnamo tarehe 24/6/2019 tulipata taarifa ya kiintelijensia kuwa kuna wahamiaji haramu waliokuwa wanasafirishwa kutoka Tanga kwenda Afrika ya Kusini kupitia mpaka wa Tunduma ndipo tukaweka mtego wa kuwanasa wasafirishaji wa wahamiaji haramu hao” amesema kamishna angela shija..

Afisa huyo wa uhamiaji mkoa wa Morogoro amesema wamefanikiwa kumkata msafirishaji wahamiaji hao ambaye alishawahi kushikwa mwaka 2014 mkoani Morogoro akifanyabiashara hiyo na akiachiliwa baada ya kulipa faini huku akitoa wito kwa wananchi kuwa na uzalendo kwa nchi yao ikiwemo kwa kushiriki kuwafichua au kutoa taarifa za kufanikisha kukamatwa kwa wahamiaji haramu ambao huingia nchini kwa malengo tofauti na kuahidi msako mkali utaendelea kuwabaini sambamba na elimu kwa wananchi ili kusaidia kuwafichua.
 Afisa Uhamiaji mkoa wa Morogoro, Angela Shija akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la kukamatwa kwa wahamiaji haramu 12 raia wa Ethiopia waliokuwa wamejificha katika pori la kijiji cha Lugono wilayani Mvomero.
Wahamiaji haramu 12 raia wa Ethiopia waliokamatwa wakiwa wamejificha katika pori la kijiji cha Lugono wilayani Mvomero.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad