HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 25, 2019

Vodacom M-Pesa kunufaika na gawio la bilioni 27 za faida ya M-Pesa

Wateja  wa Vodacom M-Pesa taktribani milioni 8, kuanzia leo watapata sehemu ya faida ya bilioni 27 ikiwa ni bonus kutoka kwenye akaunti ya M-Pesa Trust. Mtandao huo unaoongoza nchini ulitangaza kwamba kwa mwezi mmoja na nusu kuaanzia leo, wateja wake wa M-Pesa watapata sehemu yao ya gawio hilo lililopatikana kama faida ya matumizi ya huduma hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa M-Commerce Epimack Mbeteni alisema, "tunashauku ya kugawana faida hii na wateja wetu kwani wao ndio sababu ya mafanikio ya huduma ya M-Pesa. Huduma ya M-Pesa imechangia maendeleo lukuki ya watanzania na mpango huu umedhamiria kuendelea kuwapa wateja wetu faida zaidi. Wateja wote wa Vodacom ambao wamekuwa wakitumia M-Pesa watafaidika na bonus hii ya bilioni 27 ambayo itagawiwa moja kwa moja kupitia M-Pesa”.
Kuanzia sasa wateja wa Vodacom wanaweza kutuma SMS ya neno KIASI kwenda namba 15300 ili kujua kiwango gani cha faida watapokea. Baada ya kupata gawio hili, wateja wa M-Pesa wanaweza kukomboa faida hiyo kwa kuitoa kama fedha taslimu, kununua muda wa maongezi, vifurushi au kulipia bili.

"Kiasi ambacho mtu atapokea kama sehemu ya faida hiyo itategemea na idadi ya miamala aliyokuwa akifanya kwa kipindi fulani. Shughuli hizo ni kama miamala ya kuhamisha fedha, malipo ya bili mbalimbali au manunuzi ya muda wa maongezi. Napenda kuwahimiza wateja wetu kutuma SMS ili kujua ni kiasi gani cha gawio hili wanaostahili kupokea" alisisitiza Epimack.

M-Pesa inaumiliki wa soko wa asilimia 38.6% na inaongoza kwa kuwa huduma ya fedha za mkononi inayotumiwa na watanzania wengi zaidi ambao wanafanya hadi TZS 4.1 trilioni kwa mwezi. "Tumewekeza vilivyo katika M-Pesa ndani ya miaka kumi iliyopita na sasa huduma imekuwa na ufumbuzi wa kibunifu unaokidhi mahitaji ya watanzania kupitia bidhaa mbalimbali kama vile M-Koba, M-Pawa, Halal Pesa M-Pesa MasterCard na nyingine nyingi. Tunaendelea kuwa na nia ya kuboresha huduma hii kwa njia ya ubunifu huku tukishirikiana na makampuni pamoja na wavumbuzi mbalimbali ili kuendesha ajenda ya ujumuishwaji wa kifedha nchini" alimaliza Mbateni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad