HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 24, 2019

UJIO WA MAMEYA NCHINI, MWITA ATANGAZA NEEMA KWA WATANZANIA

* Awataka wafanyabiashara kutumia fursa hiyo kujitangaza zaidi.

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
MEYA wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amesema kuwa siku ya kesho June 25 wanatarajia kupokea ugeni mkubwa wa Mameya wakiongozwa na mameya kutoka katika majiji ya Texas na Albama ya nchini Marekani ikiwa ni maandalizi ya mkutano mkuu utakaofanyika mwezi Desemba mwaka huu, ambapo mkutano huo utawakutanisha mameya wenye asili ya Afrika "Black Mayors" kote duniani.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwita amesema kuwa mameya hao watakuwa nchini kwa siku 2, kuanzia Juni 25 na 26 na wataelekea Zanzibar na baadaye kurejea nchini kwa kufanya shughuli nyingine ikiwemo utalii.

Akieleza malengo ya ujio huo Mwita amesema kuwa ni kuhoji na kutaka kujua kama nchi itaweza kuwatambua kwa uraia pacha au namna yoyote ile kwa malengo ya kuwavutia wawe wawekezaji  na kuhamishia mitaji yao katika bara la Afrika.

 Pia amesema kuwa ugeni huo unakuja kwa malengo ya kuendeleza
 mahusiano bora na bara la Afrika na hiyo ni baada wamarekani hao wenye asili ya Uafrika "Wamarekani weusi"  kupoteza makazi yao na wazazi wao kuchukuliwa kama watumwa katika miaka ya 1619.

Pia amesema kuwa mameya hao wamekuja kufanya utalii ikiwemo kutembelea  Zanzibar ambako kunafahamika sana kwa usafirishaji wa watumwa.

Vilevile amesema kuwa ujio huo unafaida kwa Watanzania hasa katika kutangaza biashara za hoteli ambako inategemewa fedha nyingi zitaingizwa na amewataka watanzania kutumia nafasi hiyo adhimu kwa kutangaza biashara zao.

Mkutano mkuu wa mameya utafanyika mwezi Disemba mwaka huu ambao mameya wenye asili ya waafrika "The World Black Mayors conference" duniani kote watakutana nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad