HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 18, 2019

TASAF KUVINOA VIKUNDI VYA WANUFAIKA KUHUSU KUWEKA AKIBA NA KUKUZA UCHUMI

Wataalamu kutoka TASAF wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji kutoka Halmashauri ya Mji Njombe
Sehemu ya Wawezeshaji wakifuatilia kwa makini mada zinazotolewa juu ya uwekaji akiba na ukuzaji uchumi kwa wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini
Kaimu Meneja wa Miradi kutoka TASAF Ndg. Abdulmalik akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa warsha ya kuwajengea uwezo wawezeshaji kuhusu mpango wa kuhamasisha jamii kuweka akiba na kukuza uchumi
Wawezeshaji wakifuatilia mada
Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe Ndg. Thadei Luoga akifungua mafunzo kwa wawezeshaji kuhusu kuhamasisha wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini TASAF III kuweka akiba na kukuza uchumi.Kushoto kwakwe ni Mratibu wa TASAF ngazi ya Halmashauri Peter Magehema akifuatiwa na Afisa Ufuatiliaji wa TASAF ngazi ya Halmashauri Revocatus Rugeiyamu

……………………
Hyasinta Kissima-Afisa Habari H/Mji Njombe
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Nchini TASAF umeendelea kuwawezesha wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini kupitia mpango wa kuweka akiba na kukuza uchumi lengo ikiwa ni kuhamasisha walengwa kuunda vikundi na kuimarisha uchumi wa kaya zao.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya kuwajengea uwezo wawezeshaji ngazi ya Halmashauri kuhusu uhamasishaji wa uundwaji wa vikundi vya kuweka akiba na kukuza uchumi, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Ndg. Thadei Luoga amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu na ni vyema washiriki wakaelewa na kwenda kuwafundisha wanufaika ipasavyo ili waweze kuondokana na wimbi la umaskini.

“Wapo ambao wamekuwa wakibeza kuwa programu hii haichangii chochote. Hii sio kweli. Wananchi wamekuwa wakifanya shughuli mbalimbali za maendeleo lakini wakati mwingine kwa kukosa uelewa wa namna ya kuweka akiba na kutunza kumbukumbu zao wamekuwa wakiishia kwenye wimbi la umaskini wa kipato au lishe. 

TASAF wanatujengea uwezo ili tuweze kuwapelekea wanufaika na waweze kufanyia kazi.”Alisema Luoga
Thomas Mwakagali ambaye ni Mwezeshaji ngazi ya Halmashauri kutoka Kata ya Makowo amesema kuwa TASAF imekuwa ikitoa mafunzo hayo mara kwa mara lengo ikiwa ni kuwakumbusha wanufaika wa mpango wa TASAF kutengeneza vikundi ambavyo kupitia fedha za ruzuku wanazopokea kuweza kuweka akiba kwa ajili ya kujiimarisha kiuchumi.

“Tumekuwa tukitoa elimu hii kwa wanufaika. Kupitia fedha za ruzuku tumekuwa tukiwahamasisha juu ya uundwaji wa vikundi vya kuweka akiba na kukuza uchumi. Kupitia fedha ambazo wamekuwa wakipokea kila baada ya miezi miwili ambapo wapo walengwa wanaopokea kiasi cha Shilingi elfu ishirini, wengine thelathini ni kiasi kidogo lakini elimu hii imewajenge nidhamu ya kutunza na kuweka akiba ambapo mpaka sasa tunavikundi vyenye milioni tano, milioni mbili. Haya yote ni manufaa ya elimu hii ya akiba.”Alisema Mwakagali.

Halmashauri ya Mji Njombe ina jumla ya wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini 3381 ambapo jumla ya vikundi 123 vya akiba vimeshaundwa na kupatiwa masanduku ya kuhifadhia hela na shajara mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad