HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 18, 2019

TAMUFO yampongeza Dk Ritta Kabati

TAASISI ya Sanaa na Utamaduni ya Tanzania Music Foundations (TAMUFO) imempongeza mlezi wake Ritta Kabati kutunukiwa udaktari wa heshima kutoka Chuo Kikuu cha Afrika. Kwa mujibu wa Rais wa Tamufo, Dk Donald Kisanga wanatoa shukrani za pekee kwa mlezi wao huyo ambaye mchango wake katika maendeleo ya jamii ikiwemo Tamufo ni wa kupigiwa mfano.

Kisanga alisema umahiri wa Dk Kabati umesababisha kuteuliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalum, hivyo wanatoa wito kwa jamii ya Tanzania kuitumia ipasavyo heshima aliyoipata mwanamama huyo. "Sisi Tamufo tunapongeza uteuzi wa Dk. Kabati kwani unaendana na anayoyafanya katika jamii hususani sisi wasanii ambao tumejipanga kukua na kuendeleza kazi zetu," alisema Dk Kisanga.

Aidha Dk Kisanga alisema kutokana na ushirikiano ulio bora kati ya Tamufo na Dk Kabati, nyanja ya sanaa hapa nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla itapiga hatua zaidi ya ilivyo sasa. Mahafali ya kutunukiwa tuzo hiyo ya Udaktari yalifanyika Juni 15 jijini Lusaka Zambia ambako mahafali yake yalipambwa na bendi mahiri zilizokuwa zikiimba nyimbo mbalimbali ukiwemo wimbo wa Taifa la Tanzania.

Ritta Kabati alipata tuzo hiyo kutokana na mchango wake katika jamii ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa.
 Rais wa Tamufo, Dk Donald Kisanga akimpongeza Ritta Kabati baada ya kutunukiwa udaktari wa heshima na Chuo Kikuu cha Afrika.
Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akipongezwa na Katibu Mkuu wa Tamufo, Stella Joel.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad