HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 3, 2019

NMB YATOA NAFASI KWA WATU WATANO WENYE ULEMAVU KUJIFUNZA MAMBO MBALIMBALI

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV 

Benki ya NMB imetoa nafasi tano kwa watu wanaoishi na ulemavu kujifunza masuala tofauti ndani ya benki hiyo katika Idara zake mbalimbali kwa kipindi cha awali cha miezi mitatu. 

Benki hiyo imetoa nafasi hizo wakati wa uzinduzi wa mpango maalum ujulikanao kama 'All Inclusive' kwa kushirikiana na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na Taasisi ya CEFA inayojihusisha na watu wenye Ulemavu pamoja na Hospitali ya CCBRT ya Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Rasilimaliwatu kutoka Benki hiyo, Emmanuel Akonaay amesema wametoa nafasi hizo kwa kuangalia ujuzi,mafunzo na elimu zao ambapo watapata nafasi ya kupata mafunzo kwa vitendo katika idara tofauti za benki hiyo.

Akonaay amesema NMB inaamini uwezo wa mtu uko kwenye kipaji na sio muonekano wake wa nje, amesema wametoa nafasi hizo kwa kwa watu wa jamii hiyo kuonyesha vipaji na baadae kutoa ajira kwao pale kutakapokuwa na uhitaji.

Kwa Upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Taaluma ndani ya Rasilimali watu kutoka Benki ya NMB, Joanitha Rwegasira amesema wamepokea Watu 25 watakaopata mafunzo hayo katika masuala ya Kifedha na masuala mbalimbali yakibenki. 

Naye Mmoja wa Watu wanaopata mafunzo hayo, Mwanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Faudhia Kitenge amesema amepata nafasi yakujifunza masuala mbalimbali ya utendaji wa kibenki.

Faudhia ametoa wito kwa Taasisi nyingine kutoa nafasi kama hizo kwa Watu wenye Ulemavu ili kutoa nafasi kwa kundi hilo kuonyesha vipaji na uwezo kwa jamii.

Mwakilishi kutoka Taasisi ya CEFA, Mratibu Mkuu wa Uwezeshaji Kiuchumi, Gerald Mpangala ametoa wito kwa Taasisi mbalimbali kutoa mafunzo kama hayo kwa kuwapa Watu hao wenye Ulemavu mafunzo mbalimbali ikiwemo ya Kiuchumi, amewataka Wanafunzi watano waliopata nafasi hiyo kwenye Benki ya NMB kutumia ipasavyo nafasi hiyo kufunza.
Mtaalamu Mwandamizi wa Vipaji, Mafunzo na uendelezaji wa benki ya NMB, Edith Mwiyombela, kizungumza wakati wa ziara ya mafunzo iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa kushirikiana na Chama cha Waajiri Tanzanja (ATE), Taasisi ya CEFA na CCBRT kwa wahitimu wenye ulemavu waliyoifanya Makao makuu ya benki hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu, Emmanuel Akonaay akifafanua jambo wakati wa ziara ya mafunzo iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa kushirikiana na Chama Cha Waajiri Tanzanja (ATE), Taasisi ya CEFA na CCBRT kwa wahitimu wenye ulemavu  iliyofanyika mwishoni mwa wiki Makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Mkuu wa Kitengo Cha Taaluma ndani ya Rasilimali Watu, Joanitha Rwegasira Mrengo akieleza jambo kwenye ziara ya mafunzo iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa kushirikiana na Chama Cha Waajiri Tanzanja (ATE), Taasisi ya CEFA na CCBRT kwa wahitimu wenye ulemavu waliyoifanya  jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu Mwanadamizi Uajiri wa Benki ya NMB, Eleanor Maseke akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa ziara ya mafunzo iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa kushirikiana na Chama Cha Waajiri Tanzanja (ATE), Taasisi ya CEFA na CCBRT kwa wahitimu wenye ulemavu waliyoifanya katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad