HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 15, 2019

Watumishi NAOT Waaswa Kuzingatia Maadili

Watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) Wameaswa Kuziungatia Maadili wakati wote Wanapotekeleza majukumu yao ili kuendana na dhamira ya Serikali kufikia maendeleo endelevu na uchumi wa kati.

Akizungumza wakati akizindua Baraza jipya la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo Jijini Dodoma Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Francis Michael amesema watumishi wote wa Ofisi hiyo wanapaswa kuhakikisha kuwa wanazingatia sharia kanuni na taratibu za utumishi wa umma ili kuleta tija katika majukumu wanayotekeleza.

“ Sitarajii Wakaguzi wetu Wakawa miongoni mwa watumishi watakaokumbwa na kashfa za namna yoyote hivyo niwaase kujiepusha na vitendo vya utovu wa nidhamu,kudai na kupokea rushwa” Alisisitiza Dkt. Michael

Akifafanua amesema kuwa hatma ya makosa hayo ni kupoteza ajira na kufikishwa katika vyombo vya sheria ikiwemo mahakama ili sharia iweze kuchukua mkondo wake hali inayoweza kupelekea mhusika kufungwa jela.
Aidha, aliwataka wajumbe wa Baraza hilo kutumia fursa za Dodoma kuwa makao makuu ya Serikali kujiletea maendeleo kwa kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo ardhi.

Kwa upande wake Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Serikali Prof. Mussa Assad amesema kuwa Ofisi hiyo imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa weledi ili kutimiza lengo la kuanzishwa kwake ikiwemo kuhakikisha kuwa ripoti ya ukaguzi inatolewa kama inavyotakiwa kila ifikapo mwezi machi.
Aliongeza kuwa watumishi wa Ofisi hiyo wameendelea kujituma na kufanya kazi kwa bidii nyakati zote hali inayoonesha jinsi wanavyojitoa katika kuhakikisha kuwa kazi za ofisi hiyo zinafanyika kama inavyotakiwa.

Baraza la wafanyakazi wa NAOT linafanyika Jijini Dodoma kwa siku mbili likiwa na dhamira ya kuwaleta pamoja wajumbe kutoka katika Idara, Vitengo, Kada, baadhi ya Taasisi na vyama vya wafanyakazi likiwa ni Baraza la mwaka 2018/2019.
 Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Francis  Michael akisisitiza umuhimu  wa watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi  (NAOT) kuzingatia maadili ya utumishi wa umma wakati wa kutekeleza majukumu yao , ameyasema hayo wakati akifungua baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo Jijini Dodoma.
 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad akisisitiza umuhimu wa Baraza la Wafanyakazi  wakati wa hafla ya kufungua  Baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo Jijini Dodoma.
 Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Francis  Michael  akikata utepe kuzindua  mkataba wa huduma kwa wateja wakati wa hafla ya kufungua baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo Jijini Dodoma.
 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad akiteta jambo na Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Francis  Michael wakati wa hafla ya kufungua  Baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo Jijini Dodoma. 
 Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Francis  Michael akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi  (NAOT) mara baada ya kufungua  baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo Jijini Dodoma.

 Sehemu ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi  wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi  (NAOT) wakifuatilia hafla ya ufunguzi wa baraza hilo leo Jijini Dodoma.
 Naibu mkaguzi mkuu Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) Bi Wendi   Masoy akitoa neno  la shukrani mara baada ya uzinduzi wa  Baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo Jijini Dodoma.
Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Francis  Michael akisisitiza jambo kwa  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad leo Jijini Dodoma baada ya kuzindua Baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo.
(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad