HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 24, 2019

WANAKIJIJI CHIKONGO WASHUPALIA MAPATO NA MATUMIZI

Kamati ndogo ya kuchunguza mapato na matumizi imeundwa katika mkutano wa hadhara wa kijiji cha Chikongo baada ya Wananchi kuchachamaaa kwa kuikataa taarifa ya Serikali ya kijiji.

Sakata hilo limeibuka kwenye mkutano wa robo ya tatu ya mwaka katika Kijiji cha Chikongo kilichopo kata ya Mkoreha mbele ya Afisa Tarafa ya Mihambwe Gavana Emmanuel Shilatu baada ya Wananchi kutokuwa na imani na ripoti iliyosomwa kutowaridhisha .

Kutokana na tafran hiyo Afisa Tarafa ya Mihambwe Emmanuel Shilatu aliagiza mara moja iundwe kamati ndogo itakayopitia mapato na matumizi ya Kijiji hicho jambo ambalo liliungwa mkono na Wananchi.

Gavana huyo alitaka kamati hiyo ihusishe viongozi wa kata, Serikali ya Kijiji, baadhi ya Wananchi na wajumbe wa kamati ya ujenzi ili kumaliza utata huo na ukweli ujulikane

"Yapo madai ya mkutano mkuu wa kijiji hauitishwi kwa mujibu wa kalenda, Wananchi hawasomewi mapato na matumizi, Madai hayo ni ukiukaji wa sheria. Napendekeza iundwe kamati hapa hapa. Ipekue hesabu kisha ije na majibu ya kuridhisha" Alisema Gavana Shilatu.

Katika hatua nyingine Gavana Shilatu kupitia mkutano huo aliwataka Wakulima kuendelea na kazi zao za kilimo na wajasiliamali kuendelea kupatiwa vitambulisho vya shughuli zao.

"Mkulima ahakikishe analima, Mjasiriamali apatiwe kitambulisho. Tunahitaji kila Mwananchi awe mlinzi wa amani. Wote tukifanya kazi ndipo tutakapoinua uchumi wa nchi." alieleza Gavana Shilatu.

Katika mkutano huo wa Kijiji ulihudhuliwa na Afisa Tarafa Mihambwe, Diwani kata ya Mkoreha, Mtendaji kata na Wajumbe wa Serikali ya Kijiji cha Chikongo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad