HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 13, 2019

WAKALA WA CHAKULA, DAWA NA VIPODOZI ZANZIBAR NA WADAU WA AFYA WAJADILI MUONGOZO WA DAWA WA AFRIKA MASHARIKI

Na Miza Kona Maelezo Zanzibar
Wakala Chakula na Dawa imeanza kujadili muongozo maalum uliotolewa na Jumuiya ya Afrika Mashariki wenye lengo la kuinusuru jamii na athari zitakanazo na matumizi ya dawa ambayo hatimae husababisha madhara mbalimbali kwa wananchi.

Hayo yameelezwa na Afisa kutoka Wakala wa Dawa na Chakula Mohammed Omar kwenye Ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe katika kikao cha wadau kinachojadili hatua zinazofaa kuepukana na madhara ya dawa na vifaa tiba.

Amesema lengo la kikao hicho ni kutengeneza Muongozo ambao utawezesha kufuatilia madhara ya dawa, vifaatiba, tiba asili pamoja na chanjo ili kupata jamii yenye afya bora na kuepukana na maradhi yanayotokana na matumizi ya dawa.

Amesema muongozo huo pia utaweza kusaidia kuripoti, kuziwakilisha na kizitambua kuchunguza na kufuatilia dawa ambazo zinaleta madhara kwa jamii na kuzitafutia hatua za kuzipatia ufumbuzi kwa kutumia njia muafaka bila ya kubadilisha dhamira iliyowekwa na Jumuiya hiyo

Amefahamisha kuwa kumekuwa na matatizo makubwa ya madhara ya dawa ambazo husababisha kupata maradhi yasiyoambukiza kutokana na jamii kutotumia dawa bila ya kiwango kinachotakiwa.

“Dawa zina faida lakini pia madhara kadri unavyotumia dawa ndio madhara yanapoonekana hivyo tumeandaa muongozo wa kuweza kuzitambua dawa zenye kuleta madhara kwa jamii na kuzifanyia kazi kwa kuzifutia na kuzitambua ili kuweza kuisadia jamii”, alieleza Afisa huyo.

Alisema wameweka fomu kila kituo cha Afya na hospitali kuzitambua dawa ambazo zinaleta madhara kwa jamii kwa kila mtumiaji ambae atapata madhara baada ya kutumia ili kupata ufumbuzi na kuisadia muongozo huo kufanyakazi yake lakini changamoto kubwa iliopo urejeshaji wa fomu hizo ni mdogo.

Nae MratibuMsaidizi wa Kitengo Shirikishi Ukimwi, Homa ya Ini, Kifua Kikuu na Ukoma Issa Abeid Mussa amesema muongozo huo utaweza kujadi namna ya ufuatiliaji wa dawa na kuratibu athari zinazotokana na madhara utumiaji wa dawa

Ameitaka Wakala wa Dawa na Chakula kuangalia kwa kina na kuzifuatilia dawa zote zinazoingizwa nchini kabla ya kuzisambaza katika vituo na kuzitumia ili kuepuka madhara kwa jamii.
 MratibuMsaidizi wa Kitengo Shirikishi Ukimwi, Homa ya Ini, Kifua Kikuu na Ukoma Issa Abeid Mussa akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya uangalizi wa Dawa zikiwa sokoni katika Mkutano wa siku sita wa kujadili athari zitokanazo na dawa uliofanyika Ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.
Wadau wa Dawa na Vifaa tiba wakijadili mwangozo uliotolewa na Jumuiya ya Afrika Mashariki wenye lengo la kuhakikisha matumizi ya dawa na vifaa tiba havileti madhara kwa wananchi katika Mkutano uliofanyika Ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe. Picha na Makame Mshenga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad