HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 28, 2019

Katazo La Matumizi Ya Mifuko Ya Plastiki Lasimamisha Masomo Kwa Wanafunzi Mkoani Tabora

Na, Editha Edward-Tabora 

Wanafunzi wa Shule Mbalimbali Za sekondari zilizopo Katika Manispaa ya Tabora Mjini leo wamesitisha masomo ikiwa lengo kubwa ni kufanya Maandamano ya kuhamasisha katazo la matumizi ya Mifuko hiyo 

Hayo yamejili Mapema leo hii Katika Maandamano yaliyofanywa na Wananchi katika makundi Mbalimbali wakiwemo wajasiriamali na Wananchi wa kawaida ambao ndio watumiaji wakuu wa Mifuko hiyo

Rajabu Hamis, Magreth Yohana ni baadhi ya Wanafunzi waliojitokeza Katika Maandamano hayo ambapo wamesema wataendelea kuhamasisha wazazi wao na walezi wao ili kuhakikisha waunga mkono juhudi Za Serikali ya Awamu ya Tano

Matrida James ambae ni Mwlimu wa Shule Ya Wasichana (Tabora Girls) Amesema kuwa Wananchi wa Tabora wanalojukumu la kufahamu kuwa Mifuko ya Plastiki imepigwa Marufuku kwa Sababu inasababisha Uharibifu wa Mazingira

"Mifuko ya plastiki inasababisha Uharibifu wa Mazingira na Afya ya binadamu ambapo mifuko hii inapelekea kupata maradhi mbalimbali pia inachangia kwa vifo vya wanyama endapo watatafuna vipande vya mifuko ya Plastiki "Amesema Matrida

Kwa upande wa Wajasiriamali waliojitokeza katika maandamano hayo wametoa hisia zao kwa kuiomba Serikali kupitia Wizara husika kuhakikisha wanasimamia mfumuko wa bei katika uuzaji wa vifungashio mbadala vitakavyoletwa

Tamko la kusitisha matumizi ya mifuko ya plastiki lilitolewa na Wizara ya Mazingira na Muungano ambayo ipo chini ya Makamu wa Rais Ikiwa lengo kuu Kutunza mazingira ya nchi na Tayari Kuanzia June 1 Mwaka huu litaanza kufanya Kazi kwa Asilimia 100.
Wanafunzi wa Shule mbalimbali Za sekondari manispaa ya Tabora mjini wakionesha Mabango yanayohamasisha Uungwaji Mkono wa Katazo la Matumizi ya Mifuko ya Plastiki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad