HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 5, 2019

JAFO AMEZINDUA MADARASA MATATU KATIKA S/MSINGI MASANGANYA HUKO KISARAWE

NA MWAMVUA MWINYI, KISARAWE
Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) Suleiman Jafo amezindua vyumba vya madarasa matatu, katika shule ya msingi Masanganya ,kata ya Kibuta, wilayani Kisarawe mkoani Pwani.

Akizindua madarasa hayo ambayo yamejengwa na mkandarasi anayejenga reli ya kisasa SGR kupitia kampuni ya Yapi Merkezi kwa kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRC ) ,ameipongeza kampuni hiyo kwa kujenga madarasa hayo na kukarabati vyumba vingine vitano vya madarasa.

Jafo ,aliyataka makampuni mengine yaliyowekeza mkoani humo kuiga mfano uliofanywa na Yapi Merkezi kwa kupitia TRC kwani mkoa bado una changamoto mbalimbali kwenye sekta ya elimu .

Nae mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo alieleza, mkoa huo bado unakabiliwa na changamoto kubwa ya upungufu wa vyumba vya madarasa 3,600.

Ndikilo, aliwataka walimu na wanafunzi kutunza miundombinu hiyo ili iweze kudumu kwa kipindi kirefu.

Akitolea ufafanuzi, hali ya kielimu kimkoa, alibainisha kwamba inazidi kuimarika kwani matokeo ya darasa la la saba kwa mwaka 2017 mkoa ulishika nafasi ya 19 kati ya mikoa 26 na kwa mwaka 2018 mkoa ulishika nafasi ya 11. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad