HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 2, 2019

EAGLES SEKONDARI YAFICHUA MBINU YA KUWAJENGA WANAFUNZI

*Yajiegemeza katika kujenga maadili na kuwatumia wanasaikolojia kama mbinu mbadala ya adhabu

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MAADILI na malezi katika kuwakuza  vyema vijana katika sekta ya elimu imeelezwa kuwa ni nyenzo muhimu ya kuwajenga na kuwandaa vijana   ambao ndio nguzo kwa taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa shule ya sekondari ya wavulana Eagles iliyopo Bagamoyo Mkoani Pwani Adam Mgonde amesema kuwa katika kuhakisha zao linalotokana na elimu nchini linakuwa bora zaidi shule hiyo imeenda mbali zaidi kwa kuwa na mtaalamu wa ushauri nasaha (mwanasaikolojia) pamoja ushauri na kuwahudumia watoto wote shuleni hapo.

Amesema kuwa watoto wa kipindi hiki ni tofauti sana kwa kuwa wanajua mambo mengi kutokana na maendeleoya sayansi na teknolojia na kuwaadhibu wanapokosea sio suluhisho bali ni kuwaelekeza kuhusiana na maadili mema pamoja na malezi.

Aidha amesema kuwa baada ya serikali kuridhia mabadiliko kadhaa ya muundo wa shule hiyo rasmi wameandaa tahasusi mpya kabisa ambazo hazikuwahi kutolewa nchini pamoja na masomo na hiyo inakuja baada ya malengo ya taifa kuelekea uchumi wa viwanda ambao unahitaji wataalamu wa kutosha.

Akieleza kuhusu masomo na tahasusi zilizoongezwa Mgonde amesema kuwa masomo ya kilimo yameanza kutolewa shuleni hapo na kwa kushirikiana na ubalozi wa Ufaransa wameanzisha somo la Kifaransa mwaka huu na ifikapo Julai tahasusi ya KLF (Kiswahili, English Language na French) itatolewa shuleni hapo.

Kwa upande wake mwalimu wa biashara na mkuu wa Masoko shuleni hapo Gadi Lameck amesema kuwa tahasusi mpya za masomo ya sayansi yanayojumisha masomo ya kompyuta zitatolewa kwa mara ya kwanza shuleni hapo na hiyo ni katika kwenda sambamba na matakwa ya taifa ya kujenga uchumi imara wa viwanda na wao kama Eagles High School wanatoa mafunzo kwa kilimo kwa utendaji ili kuzalisha vijana wenye mawanda mapana ya kusaidia taifa.

Katika kukuza sekta ya elimu nchini imeshauriwa kukuza malezi ya vijana, maadili, ubunifu na afya njema ili kutimiza ndoto za kizazi cha kesho na nguzo ya taifa.
 Mkuu wa shule ya sekondari ya wavulana Eagles Adam Mgonde (katikati) akizungumza na wanahabari kuhusiana na kukuza sekta elimu, leo jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa shule ya Sekondari ya wavulana Eagles, Adam Mgonde wakati akiwasilisha taarifa ya uboreshwaji wa sekta ya elimu katika shule hiyo leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad