HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 9, 2019

Chelsea na Aresenal kutinga fainali EUROPA League?

Baada ya mchezo wa ligi ya mabingwa jana usiku kwa staili ya aina yake, na kupelekea fainali ya waingereza kwenye shindano hilo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2008. Usiku wa leo Chelsea na Arsenal watacheza michezo ya marudiano katika nusu fainali ya EUROPA huku wakiwa na matumaini ya kucheza fainali ya waingereza mwisho wa mwezi. Mara ya mwisho timu za Uingereza kukutana kwenye fainali ya EUROPA (kipindi hicho UEFA Cup) ilikuwa mwaka 1972, ambapo Wolverhampton Wanders walicheza dhidi ya Tottenham Hotspur na Spurs kushinda 3-2 baada ya michezo miwili (kwa muundo wa zamani).

Miaka 47 baadaye, Chelsea na Arsenal wana nafasi ya kufanya hivyo na kuandika historia. Itakuwa ni mara ya pili tu kwa timu za jiji moja kugombania Ubingwa wa Ulaya katika fainali, mara ya kwanza walikuwa mahasimu wa jiji la Madrid. Arsenal wanasafiri kuelekea Valencia wakiwa wanaongoza kwa 3-1, huku Chelsea watakuwa nyumbani baada ya kupata goli la ugenini katika mchezo wa kwanza uliomalizika kwa sare 1-1 dhidi ya Eintracht Frankfurt.

Kocha wa Arsenal Unai Emery, ambaye alishuhudia matumaini ya timu yake kushiriki ligi ya mabingwa mwakani yakiyeyuka baada ya timu yake kulazimishwa sare na Brighton kwenye mchezo wa ligi Jumapili iliyopita hivyo nafasi ya pekee ni kushinda taji la Europa. "Tuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye Europa na tutajaribu kufanya hivyo,” alisema Emery ambaye alishinda taji hilo mara tatu mfululizo akiwa na Sevilla.

Naye mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon Pierre Emerick Aubameyang anatamani kucheza na Eintracht Frankfurt kwenye fainali, kuliko kucheza na mahasimu wao, Chelsea. “Siwataki Chelsea.  “Tunawafahamu ni timu nzuri lakini nadhani sisi tutaingia fainali kwanza na ningependa tucheze dhidi ya Frankfurt kwa sababu Chelsea tumeshacheza nao [kwenye ligi]. Nafahamu Frankfurt ni wazuri sana kama sote tutaingia fainali utakuwa mchezo mzuri sana. Tunataka kushinda taji hili kwa sababu ndilo lengo letu tangu mwanzo wa msimu” 

Kocha wa Chelsea alizomewa na mashabiki wao kwenye mapumziko katika mechi dhidi ya Watford Jumapili iliyopita, lakini walirudi vizuri kipindi cha pili na kushinda kwa mabao 3-0 na kujihakikishia nafasi ya nne kwenye msimo wa ligi. Mchezo wa Valencia dhidi ya Arsenal utapigwa saa 4:00 Usiku na kurushwa Mubashara kupitia StarTimes Sports Premium HD, huku ule wa Chelsea vs Eintracht Frankfurt ukipigwa muda huo huo na kuonyeshwa kupitia StarTimes World Football HD.

Chaneli zote zinapatikana katika kifurushi cha UHURU (Antenna) kwa Tsh 18,000 tu kwa mwezi na SMART (Dish) kwa TSh 21,000 kwa mwezi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad