HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 4, 2019

WIKI YA UTAFITI ILETE TIJA YA MAENDELEO KWA TAIFA - DR MBUNA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

CHUO Kikuu Kishirikishi Dar es Salaam (DUCE) wamezindua maadhimisho ya tano ya wiki ya utafiti wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam .

Akizindua maadhimisho hayk yenye kauli mbiu ya  Utafiti kwa maendeleo Jumuishi na Endelevu (Research for inclusive and Sustainable Development)  Naibu Mkuu wa Chuo cha DUCE (Taaluma) Dr Julius Mbuna amewapongeza wanataaluma wote kufanikisha shughuli hiyo.

Dr Mbuna amesema, kufanya tafiti ni moja ya shughuli muhimu za chuo kwani Chuo cha DUCE kilianzishwa kwa lengo la kufanya shughuli kuu tatu ambazo ni kufundisha, kufanya utafiti na kutoa huduma kwa jamii.

Amesema, Chuo kipo katika mchakato wa kupitia sera ya utafiti (Research Policy and Operational Procedures) na sera ya huduma za ushauri ( Consultancy Policy and Operational Procedures) pamoja na kudumisha mahusiano mapya ya vyuo na asasi mbalimbali ndani na nje ya nchi ili kutafuta mianya ya wanataaluma wa chuo kushirikiana na wengine katika shughuli za Kitafiti.

Pia, ameeleza kuanzishwa kwa digrii za umahiri ni mkakati wa mahususi wa kuhakikisha wanataaluma wanafanya tafiti kwani ni moja ya kigezo cha kuhitimu digrii hiyo ni kufanya utafiti utakaosimamiwa na wanataaluma wetu, wanataaluma watawezeshwa kushirikiana kiutafiti na wanafunzi wao.

“Chuo kimefanya mengi kuhakikisha kuwa shughuli za utafiti zinafanyika hapa chuoni na kuchangua katika maendeleo ya taifa na kutoa wito kwa wahadhiri na wafanyakazi wote wa chuo kuongeza bidii zaidi katika kuandaa mapendekezo ya kufanya tafiti zitakazoingizia fedha chuo.

Aidha, chuo kimeendelea kuchapisha jarida lake la kimataifa liitwalo Journal Of Education, Humanities and Sciencena wanaendelea kugharamia kila kitu katika uchapishaji wa jarida hilo ikiwa ni uthibitisho wa dhamira ya dhati ya chuo kwenye kuendeleza shughuli za utafiti.

Kwa upande wa Mkuu wa kitengo cha Utafiti wa NECTA Dr Alfred Mdima amesema kuwa tafiti ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi na ametoa pongezi kwa DUCE kwa kupiga hatua kwenye masuala ya utafiti wa masuala mbalimbali.

Baada ya kuzindua maadhimisho ya tano ya wiki ya utafiti, Dr Mbuna alitembelea mabanda mbalimbali yaliyoandaliwa na wanataaluma waliofanya tafiti za aina mbalimbali kwa muda wa siku mbili April 3 na 4.
Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam DUCE Dr Julius Mbuna akitembelea mabanda ya maonesho ya wanataaluma waliofanya tafiti mbalimbali baada ya ufunguzi  maadhimisho ya wiki ya utafiti ya Chuo Kikuu Dar es Salaam yanayofanyika kwa siku mbili April 3 hadi 4 kwenye Chuo cha DUCE, Wa pili Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Utafiti wa NECTA Dr Alfred Mdima.

 Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam DUCE Dr Julius Mbuna akitembelea mabanda ya maonesho ya wanataaluma waliofanya tafiti mbalimbali baada ya ufunguzi  maadhimisho ya wiki ya utafiti ya Chuo Kikuu Dar es Salaam yanayofanyika kwa siku mbili April 3 hadi 4 kwenye Chuo cha DUCE, Wa pili Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Utafiti wa NECTA Dr Alfred Mdima.
 Mkuu wa Kitengo cha Utafiti wa NECTA Dr Alfred Mdima akizungumza jambo baada ta ufunguzi wa Wiki ya utafiti kwenye chuo Kikuu Kishirikishi DUCE yatakayofanyika kwa siku mbili April 3 na 4.
Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam DUCE Dr Julius Mbuna akisikiliza mdahalo wa elimu baada ya ufunguzi  maadhimisho ya wiki ya utafiti ya Chuo Kikuu Dar zes Salaam yanayofanyika kwa siku mbili April 3 hadi 4 kwenye Chuo cha DUCE

Wahadhiri na wanataaluma mbalimbali wakifuatilia mdahalo wa masuala ya elimu ya ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya utafiti yanayofanyika kwa siku mbili kwenye Chuo Kikuu Kishirikishi DUCE.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad