HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 22, 2019

WAZIRI WA AFYA AWATAKA WATANZANIA KUFUATA MAELEKEZO YA WATOA HUDUMA ZA AFYA PINDI WAUGUAPO MALARIA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jisnia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema mapambano dhidi ya Malaria yanaonesha mafanikio makubwa kutokana na kushuka kwa Maambukizi hayo kutoka aslimia 14.5 mwaka 2015 hadi kufikia aslimia 7 mwaka huu.

Waziri Ummy amesema licha ya kushuka kwa maambukizi hayo lakini bado kuna mikoa kadhaa ambayo bado maambikizi ya ugonjwa wa Malaria yapo juu na hivyo kutoa wito kwa wadau kuongeza jitihada katika kuutokomeza kabisa ugonjwa huo.

Mhe. Waziri ameitaja mikoa ambayo maambukizi ya ugonjwa Malaria yapo juu kuwa ni pamoja na Mara, Geita, Kagera, Mtwara, Lindi na Ruvuma ambapo amewataka wananchi kuongeza jitihada katika kupunguza kiwango cha Ugonjwa huo.

"Licha ya jitihada zinazofanywa kumaliza ugonjwa huu lakini bado jitihada zinahitajika zaidi katika kufikia lengo la ZERO MALARIA ifikapo 2030". Amesisitiza Mhe. Ummy.

Kuhusiana na maadhimisho ya mwaka huu ya siku ya Malaria Duniani, Mhe. Ummy amewataka wananchi wote kushiriki katika kufikia lengo la Zero Malaria kwa kutomeza mazalia ya Mbu, kutumia vyandarua vilivyowekwa Dawa, kwenda hospitalini pindi wanapohisi wana viashiria vya Malaria na kumaliza dozi kama watakavyo elekezwa na watalaamu wa Afya.

"Wito wangu kwa watanzania wote ni kuhakikisha wanafuata maelekezo ya watoa huduma za afya pindi wauguapo Malaria na pia kuweka mazingira yao safi ili kukabiliana na mbu waenezao Ugonjwa wa Malaria" Alisema Mhe. Waziri.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya Malaria kwa Mwaka huu ni ZIRO MALARIA INAANZA NA MIMI huku maadhimisho ya Siku ya Malaria hapa nchini yanatarajiwa kufanyika April 25, Mkoani Lindi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad