HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 25 April 2019

Waziri wa Afya ashiriki kwenye ungawaji wa vyandarua ikiwa ni moja ya maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani

Waziri wa Afya ashiriki kwenye ungawaji wa vyandarua ikiwa ni moja ya maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,amesema kuwa Serikali imeweza kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Malaria kwa asilimia 50 kutoka asilimia 14 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 7.

Hayo ameyasema leo wakati wa kugawa vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja na nusu katika hospitali ya Wilaya ya Dodoma.

Aidha,amesema kuwa halmashauri kutenga fedha za ndani kwa ajili ya kununua viuwadudu ikiwa ni katika kupambana na maambukizi ya Malaria katika maeneo yao.

Waziri Ummy amesema kuwa kwa kipindi cha miaka 2 ya utawala wa Rais John Magufuli, Tanzania imeweza kupunguza maambukizi ya Malaria kwa asilimia 50 kutoka wastani wa asilimia 14 mwaka 2016 hadi kufikia asilimia 7.

Hata hivyo amesema kuwa serikali imekuwa na mikakati mingi ya kupambana na maambukizi wa ugonjwawa malaria ambayo yamekuwa ikiuwa Watanzania wengi kuwa mbali na kugawa vyandarua pia wanapulizia dawa katika mikoa yenye kiwango kikubwa cha maambukizi.

”Serikali imenunua takribani lita 60,000 ya viuawadudu kwa ajili ya kuua mazalia ya mbu na kuzigawa katika mikoa yenye maambukizi makubwa ya malaria kama vile Mkoa wa Kagera, Geita, Kigoma, Lindi na Mtwara lakini pia niwaombe wananchi kutunza mazingira ili kujiepusha na mbu waenezao malaria,” amesisitiza Mwalimu

Aidha, Mwalimu alisema mkakati wa serikali ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2020 angalau wajawazito 80 kati ya 100 waweze kuhudhuria kiliniki angalau mara nne hivyo kutoa fursa ya kufanyiwa vipimo mbalimbali ikiwamo malaria.

Kwa upande wake mratibu wa ugonjwa wa malaria mkoa wa Dodoma, Fransis Bujiku amesema kuwa Mkoa huo umefanikiwa kupunguza kiwango cha maambukizi ya malaria kutoka asilimia 1 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 0.6 kwa sasa.
Bujiku amesema kuwa kwa pamoja wamefanikiwa kwa kutuna mazingira ikiwa ni pamoja na kunyunyiza dawa ya kuua mbu kipindi cha masika na kufukia madimbwi yote yanayotuamisha maji pamoja na kuwahamasisha wananchi kulala kwenye vyandarua.

Siku ya malaria duniani inafanyika kesho ambapo kitaifa itafanyikia mkoani Lindi ikiwa na kauli mbiu isemayo Ziro malaria inaanza na mimi .
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwapongeza baadhi ya wanaume ambao waliwaleta watoto klinik wakati wa kugawa vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja na nusu katika hospitali ya Wilaya iliyopo Makole jijini Dodoma.Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akigawa vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja na nusu katika hospitali ya Wilaya ya Makole jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akionesha nchandarua kwa akina mama wajawazito (hawapo pichani) wakati wa kugawa vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja na nusu katika hospitali ya Wilaya iliyopo Makole jijini Dodoma. 


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akisalimia na baadhi ya viongozi wa wilaya ya mkoa wa Dodoma alipowasili kwa ajili ya kugawa vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja na nusu katika hospitali hiyo iliyopo Makole jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa kugawa vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja na nusu katika hospitali ya Wilaya iliyopo Makole jijini Dodoma.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa na ambaye ni mratibu wa Malaria mkoa wa Dodoma, Francis Bujiku,akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma
Sehemu ya akina mama wajawazito wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (hayupo pichani) wakati wa kugawa vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja na nusu katika hospitali ya Wilaya iliyopo Makole jijini Dodoma.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad