HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 8, 2019

WAZIRI LUKUVI ATOA NENO KWA MABENKI MAONESHO YA NMB NYUMBA DAY JIJINI ARUSHA

WAZIRI wa Ardhi Nyumba Maendeleo na Makazi ,William Lukuvi,amezitaka Taasisi za Kifedha hapa nchini ikiwemo Benki kuwawezesha wananchi wa hali ya chini kupata mikopo ya nyumba kwa riba nafuu.

Aidha amezitaka taasisi hizo za kifedha kushirikiana na kampuni za ujenzi ili kuwasaidia wananchi wanaochukua mikopo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba,kumiliki nyumba kwa gharama nafuu.

Waziri Lukuvi aliyasema hayo jijini Arusha katika maonyesho ya NMB Nyumba Day,yaliyofanyika jijini hapa na kukutanisha wateja na watoa huduma katika ujenzi na uuzaji wa nyumba ambapo Benki ya NMB inatoa huduma ya mikopo kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kumiliki nyumba.

Amesema kuwa taasisi za fedha zinazotoa mikopo ya nyumba zinatakiwa kutafuta namna ya kuwasaidia wananchi ili kuweza kumudu na kupata nyumba kwa gharama nafuu.

"Ili gharama za ujenzi wa nyumba za Tanzania zisiwe za ghali taasisi za kifedha kuweni na mpango mahsusi,endelevu na ulio rahisi wa kumkopesha mtu nyumba,ili wananchi wa hali ya chini kupata mikopo kwa riba nafuu na mshirikiane na kampuni za ujenzi ili kuwasaidia wananchi wanaochukua mikopo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba,kumiliki nyumba kwa gharama nafuu," alisema

Waziri Lukuvi aliipongeza Benki ya NMB kwa kuanzisha mikopo hiyo ambapo ni miongoni mwa Benki zilizopo hapa nchini ambazo zinashirikiana na wadau wengine kuhakikisha wananchi wanapata mikopo kwa riba nafuu na kuwawezesha kumiliki nyumba za makazi.

Awali Kaimu Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati kutoka Benki ya NMB,Salie Mlay,anasema benki hiyo imekuwa baina ya wananchi na serikali katika kuwawezesha wananchi ili wapate makazi bora. WAZIRI wa Ardhi Nyumba Maendeleo na Makazi ,William Lukuvi,amezitaka Taasisi za Kifedha hapa nchini ikiwemo Benki kuwawezesha wananchi wa hali ya chini kupata mikopo ya nyumba kwa riba nafuu.

Aidha amezitaka taasisi hizo za kifedha kushirikiana na kampuni za ujenzi ili kuwasaidia wananchi wanaochukua mikopo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba,kumiliki nyumba kwa gharama nafuu.

Waziri Lukuvi aliyasema hayo jijini Arusha katika maonyesho ya NMB Nyumba Day,yaliyofanyika jijini hapa na kukutanisha wateja na watoa huduma katika ujenzi na uuzaji wa nyumba ambapo Benki ya NMB inatoa huduma ya mikopo kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kumiliki nyumba.

Amesema kuwa taasisi za fedha zinazotoa mikopo ya nyumba zinatakiwa kutafuta namna ya kuwasaidia wananchi ili kuweza kumudu na kupata nyumba kwa gharama nafuu.

"Ili gharama za ujenzi wa nyumba za Tanzania zisiwe za ghali taasisi za kifedha kuweni na mpango mahsusi,endelevu na ulio rahisi wa kumkopesha mtu nyumba,ili wananchi wa hali ya chini kupata mikopo kwa riba nafuu na mshirikiane na kampuni za ujenzi ili kuwasaidia wananchi wanaochukua mikopo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba,kumiliki nyumba kwa gharama nafuu," alisema

Waziri Lukuvi aliipongeza Benki ya NMB kwa kuanzisha mikopo hiyo ambapo ni miongoni mwa Benki zilizopo hapa nchini ambazo zinashirikiana na wadau wengine kuhakikisha wananchi wanapata mikopo kwa riba nafuu na kuwawezesha kumiliki nyumba za makazi.

Awali Kaimu Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati kutoka Benki ya NMB,Salie Mlay,anasema benki hiyo imekuwa baina ya wananchi na serikali katika kuwawezesha wananchi ili wapate makazi bora. 
Meneja Utawala na Fedha wa Elerai Construction LTD – John Tarimo akitoa maelezo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi – William Lukuvi alipotembelea maoneyesho ya Nyumba yaliyoandaliwa na NMB Bank mwishoni mwa Juma jijini Arusha. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Wateja wadogo na wa kati wa NMB – Salie Mlay na Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini – Aikansia Muro

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi – William Lukuvi akisalimiana na Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini – Aikansia Muro muda mfupi kabla ya kufungua rasmi siku ya Nyumba ya NMB jijini Arusha mwishoni mwa juma. Anayeangalia ni Mkuu wa Wateja Wadogo na Wa Kati wa NMB Bank – Salie Mlay.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi – William Lukuvi akisalimiana na Meneja Mahusiano Biashara ya Serikali wa Kanda ya Kaskazini – Christabel Hiza muda mfupi kabla ya kufungua rasmi siku ya Nyumba ya NMB jijini Arusha mwishoni mwa juma.

WAZIRI wa Ardhi Nyumba Maendeleo na Makazi ,William Lukuvi,maonesho ya NMB Nyumba Day,yaliyofanyika jijini Arusha akimsikiliza mmoja wa Wadau wa Maonesho hayo wakati wa maonesho hayi yaliyowakutanisha wateja na watoa huduma katika ujenzi na uuzaji wa nyumba ambapo Benki ya NMB inatoa huduma ya mikopo kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kumiliki nyumba.Pichani kulia ni Kaimu Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati kutoka Benki ya NMB,Salie Mlay.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi – William Lukuvi akiongea kwenye uzinduzi rasmi wa siku ya Nyumba ya NMB iliyofanyika Jijini Arusha mwishoni mwa juma. Siku ya Nyumba ya NMB ni maonyesho yenye lengo la kuwaleta pamoja wateja na makampuni ya kuuza nyumba ili kuona miradi waliyonayo na gharama kabla ya kununua kupitia benki ya NMB.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad