MWENYEKITI
wa klabu ya wafanyabiashara wa NMB Kisiwani Pemba Abdalla Ali Said,
akimkabidhi cheti meneja wa NMB Tawi la Pemba Ahmed Nassor, kwa niaba ya
mfanyabiashara Abdalla Nassor Abdalla, wakati wa hafla ya uzinduzi wa
klabu ya wafanyabiashara hafla iliyofanyika mjini Chake Chake.
MWENYEKITI wa klabu ya Wafanyabiashara wa NMB Kisiwani Pemba Abdalla Ali Said, akimkabidhi cheti cha shukurani mmoja wa wafanyabiashara na mteja wa benk ya NMB Pemba, Mwanakhamis Khamis, wakati wa hafla ya uzinduzi wa klabu ya wafanyabiashara hafla iliyofanyika mjini Chake Chake.
MKUU
wa Wilaya ya Chake Chake Rashid Hadid Rashid (kushoto), akisalimiana na
mwenyekiti wa klabu ya wafanyabiashara wa NMB Kisiwani Pemba, Abdalla
Ali Said (Ngonda) baada ya kuchaguliwa kwake na wafanyabiashara wakati
wa uzinduzi wa klabu ya wafanyabiashara Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,
PEMBA)
MWENYEKITI
Mteuliwa wa klabu ya wafanyabiashara ya NMB Kisiwani Pemba Abdalla Ali
Said (Ngonda), akizungumza na wafanyabiashara katika mkutano wa uzinduzi
wa klabu hiyo, mkutano uliofanyika mjini Chake Chake.
MKUU
wa Wilaya ya Chake Chake Rashid Hadid Rashid, akizungumza na
wafanyabiashara wa Pemba, wakati wa uzinduzi wa klabu ya wafanyabiashara
wa NMB Pemba, uzinduzi huo uliofanyika mjini chake chake.
MENEJA
wa NMB kanda ya Dar es Salam na Zanzibar, Badru Iddi akizungumzia
malengo ya Benk ya NMB kanda yake kwa mwaka 2019, wakati wa uzinduzi wa
klabu ya wafanyabiashara wa NMB Pemba, hafla ya uzinduzi huo uliofanyika
mjini Chake Chake.
MWAKILISHI
kutoka NMB Loelia Kibasa, akiwasilisha mada kuhusu NMB na Idara ya
biashara, wakati wa ufunguzi wa klabu ya wafanyabiashara wa NMB kisiwani
Pemba, halfa iliyofanyika mjini Chake Chake.
MKUU
wa Wilaya ya Chake Chake Rashid Hadid Rashid (kushoto), akisalimiana na
mwenyekiti wa klabu ya wafanyabiashara wa NMB Kisiwani Pemba, Abdalla
Ali Said (Ngonda) baada ya kuchaguliwa kwake na wafanyabiashara wakati
wa uzinduzi wa klabu ya wafanyabiashara Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,
PEMBA)
MKUU
wa Wilaya ya Chake Chake Rashid Hadid Rashid, amesema kuwa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar, inaunga mkono juhudi mbali mbali zinazochukuliwa
na benki ya NMB, katika kuwaunganisha wafanyabiashara wa Kisiwa cha
Pemba, jambo linaloweza kupelekea kuongezeka kwa mapato ya nchi.
Alisema
wafanyabiashara ni watu muhimu katika maendeleo ya uchumi wa Zanzibar
na Tanzania kwa ujumla, katika suala zima la kukusanya mapato.
Alisema
malengo ya Serikali ya awamu ya saba ya Mapinduzi ya Zanzibar ni
kuhakikisha, inaboresha mapato ya serikali kupitia kodi na kuziba mianya
yote ya ukwepaji wa kodi, ambayo husababisha upotevu wa mapato ya
serikali hali inayopelekea kuzoretesha maendeleo ya nchi.
Mkuu
huyo wa Wilaya ya aliyaeleza hayo, mjini chake chake wakati wa uzinduzi
wa klabu ya wafanyabiashara wa Pemba, ikiwa ni klabu ya kwanza kisiwani
hapa kuanzishwa na NMB.
“Muunganiko
huu pia utaweza kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara, katika suala la kodi
na jinsi ya kutunza fedha, jambo hili ni muhimu litaweza kusaidia
malengo ya wafanyabiashra, ili kuweza kujengewea uwelewa katika suala
zima la ulipaji wa kodi”alisema.
Aidha
Mkuu huyo wa Wilaya alisema, kuanzishwa kwa klabu hiyo itaweza kutoa
mwangaza kwa wafanyabiashara, kupata mafunzo mbali mbali ya biashra,
pamoja na kuelimishwa juu ya utunzaji wa kumbukumbu za biashara, masoko,
huduma nzuri kwa wateja, upangaji wa bei, sheria za biashara na
mahesabu ya fedha.
Aidha
aliwataka wafanyabiashara kufanya utafiti kwa kina wa biashara
wanayotaka kuifanya, kabla ya kuomba mkopo ili fedha wanazopatiwa waweze
kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa, pamoja na benki kufuatilia
wafanyabiashara waliowapatia mikopo na kujuwa biashara zao ipasavyo.
Meneja
wa NMB kanda ya Dar es Salam Badru Iddi, alisema NMB imeamua kuwafikia
wananchi wote wa kipato cha chini Tanzania nzima, kwani mwaka 2018
walifungua klabu za wafanyabiashara 50 Tanzania na mwaka 2019 mikakati
yao ni kufungua klabu 36 Tanzania ikiwemo ya Kisiwani Pemba.
No comments:
Post a Comment