HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 29 April 2019

USAJILI LAINI ZA SIMU KWA KUTUMIA ALAMA ZA VIDOLE, WANANCHI WOTE KUFIKIWA.

Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv, Morogoro

Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Kanda ya Mashariki imesema kuwa wananchi wote wenye laini za simu za simu watafikiwa na huduma ya usajili wa laini za simu kwa vitambulisho vya Uraia na alama za vidole na watoa huduma wa kampuni za simu nchini.

Hayo yamesemwa kutokana na kuibuka kwa sintofahamu ya namna wananchi watakavyofikiwa na watoa huduma kwa ajili ya kusajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole na kitambulisho cha uraia kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Mamlaka hiyo imewatoa hofu wananchi wote na kuwahakikishia kwamba watafikiwa na watoa huduma za mawasiliano.

Akizungumza katika Mnada wa Dakawa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero amesema wananchi wote watapata usajili wa laini zao kwa kutumia alama za vidole kwa kuwa na vitambulisho vya taifa.

Mhandisi Odiero amesema kazi yao ni kutoa elimu kwa wananchi wote hivyo watawafikia kwa njia yoyote kuhakikisha wananchi hawapati changamoto wakati wa usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole.

Amesema usajili ni jitihada za Serikali katika kuhakikisha usalama wa watumiaji wa huduma za Mawsiliano kutokana na changamoto kwa baadhi ya watumiaji kutumia mawasiliano kinyume na utaratibu uliowekwa lakini kwa sasa ni kitambulisho kimoja tu ambapo mtu akifanya uharifu ni rahisi kumfikia na hatua zitachukuliwa.

Mhandisi Odiero amesema awali TCRA iliruhusu vitambulisho vingi hata barua za Serikali za Mtaa katika kusajili hali iliyofanya baadhi ya watumiaji kukiuka taratibu ikiwemo kudanganya na kutoa taarifa za uongo wakati wa usajili na hivyo na kutoa mwanya hata kwa wahali kutumia vitambulisho hivyo kujisajili na kufanya utapeli wa kujipatia kipato kisichokuwa halali.

Naye Eng. Robson Shaban (Mhandisi mwandamizi wa Mamlaka hiyo) ameasihi wananchi ambao tayari wana vitambulisho vya Uraia kusajili mapema (Ifikapo tarehe 01/05/2019 ambayo ndio mwanzo wa Usajili) laini zao na sio kusubiri mwisho na kuonekana usajili una changamoto wakati muda ulikuwepo na wakashindwa kufanya hivyo.

Katika Mnada huo watu wengi waliuza maswali na kujibiwa na maofisa kutika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Kanda ya Mashariki. Mamlaka inaendelea kuwaelimisha watumiaji juu ya umuhimu wa zoezi hilo.
 Mhandisi Mwandamizi wa TCRA Kanda ya Mashariki Robson Shaban akiwapa maelezo ya kitabu cha muongozo wa mawasiliano katika Mnada wa Dakawa mkoani Morogoro.
Mhandisi Mwandamizi wa TCRA Kanda ya Mashariki Robson Shaban akitoa elimu ya usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole katika Mnada wa Dakawa mkoani Morogoro.
 Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mfumo mpya wa usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole katika Mnada wa Dakawa mkoani Morogoro.
 Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero akimpa maelekezo mwananchi wakati wa otoaji wa elimu ya namna ya usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole katika Mnada wa Dakawa mkoani Morogoro.

Afisa wa TCRA Kanda ya Mashariki Annastella Mchomvu akitoa maelezo kwa mwananchi katika Mnada wa Dakawa mkoani Morogoro. 

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad