HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 1, 2019

Ubungo Islamic wapata elimu ya kuomba mkopo wa elimu ya juu

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema imeweka utaratibu wa kutembelea Wanafunzi  wa Kidato cha Sita katika Shule za Sekondari ili kutoa elimu ya namna ya kuomba Mikopo katika Bodi hiyo. 

Akizungumza na Wanafunzi wa Kidato cha Sita katika Shule ya  Sekondari ya Ubungo Islamic  Afisa Mwandamizi Bodi hiyo Josephat Bwathondi amesema kuwa bodi iko kwa kazi moja ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wenye uhitaji kwa ajili ya elimu  ya juu ambapo kukosekana kwa chombo  hicho baadhi ya watanzania wangekosa elimu ya juice kutokana uchumi walio nao. 

Amesema kuwa lengo la kuwafikia Wanafunzi wa shule hiyo ni kwa ajili ya kuwapa namna ya uombaji mikopo  na taarifa  zinazohitajika katika uambaji mikopo.

Aidha amesema taarifa za msingi katika maombi hayo ni vyeti vya kuzaliwa kwa Wanafunzi, Wazazi, Kama mwanafunzi kafiwa na mzazi kuwepo kwa cheti cha kifo katoka kwa Wakala wa Udhamini, Ufilisi, Usajili wa Vifo na Vizazi (RITA).
Amesema utaratibu  hapo nyuma haukuwepo lakini wameona ni muda mwafaka wa kutoa elimu ya uoambaji Mikopo. 
Nae Afisa wa Urejeshaji Mikopo wa  Bodi hiyo Emmanuel Mtavangu amesema kuwa katika  kuwapa elimu ya uombaji  Mikopo pia lazima watambue kuwa Mikopo hiyo inarejeshwa kwa ajili ya kusomesha wahitaji wengine.
 Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Josephat Bwathondi akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Ubungo Islamic wakati walipokwenda kutoa elimu ya uombaji mikopo katika shule hiyo jijini Dar es Salaam.
 Wanafunzi Wasichana wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Ubungo Islamic wakisikiliza mada za Bodi ya Mikopo ilipokwenda kutoa elimu ya uombaji mikopo katika Sekondari hiyo.
 Wanafunzi Wavulana wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Ubungo Islamic wakisikiliza mada za Bodi ya Mikopo ilipokwenda kutoa elimu ya uombaji mikopo katika Sekondari hiyo.
Afisa wa Urejeshaji Mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Emmanuel Mtavangu akitoa maelezo ya taratibu za Urejeshaji mikopo baada ya kuhitimu shahada ya kwanza wakati Bodi ilipokwenda kutoa elimu ya uombaji mikopo katika Shule ya Sekondari ya Ubungo Islamic jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad