HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 1, 2019

KWA HILI TAASISI YA WAJIBU INASTAHILI PONGEZI

 *Somo la jaji Sammata kwa wanasheria kukomesha kabisa kansa ya rushwa

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii

TAASISI ya Wajibu nchini inayoshughulika na fikra ya uwajibikaji kwa umma imeendelea kutoa mafunzo kwa watu wa kada mbalimbali kuhusiana na masuala ya uwajibikaji na uadilifu.

Moja ya midahalo mikubwa ni ile iliyotolewa na jaji mkuu mstaafu na mkuu wa chuo cha Mzumbe Barnabas Sammata katika Chuo kikuu cha Dodoma na Chuo cha sheria nchini kilichopo jijini Dar es salaam na katika midahalo hiyo jaji Sammata alitoa mada kuhusiana na mapambano dhidi ya rushwa kwa kueleza kuwa rushwa ni kansa inayosababisha kutoweka kwa imani ya raia juu ya demokrasia .

Akiwa katika chuo cha sheria Jaji Sammata aliishukuru taasisi ya Wajibu  na uongozi wa Chuo cha Sheria kwa heshima waliyompa hasa kwa kutoa mada na kuwanoa wanasheria hao kuhusiana na mapambano dhidi ya rushwa ambayo imekuwa adui zaidi kwa ustawi wa wananchi wakati wa amani  kuliko wakati wa vita.

Jaji Sammata alieleza kuwa rushwa katika nchi inatakiwa ishughulikiwe kwa karibu sawasawa na inavyoshughulikiwa suala la uhaini na vijana lazima wawe mstari wa mbele katika kupinga rushwa.

Sammata alieleza kuwa ili kukabiliana na kansa ya rushwa lazima ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka na TAKUKURU kuhakikisha nini kifanyike ili kumwokoa mnyonge kutoka kwenyejanga hilo.

"Rushwa si kansa iliyoanza jana au juzi,kwa mujibu wa biblia ilikuwepo tangu wakati wa yesu miaka ipatayo zaidi ya elfu mbili iliyopita, Korani inakemea sana uovu huo" alieleza Sammata huku akisema kuwa sababu za kupokea rushwa ni nyingi ikiwemo kuharakisha kupata huduma, kupata zaidi ya unachostahili pamoja na kupata kile ambacho mtu ana haki nacho.

Vilevile alieleza madhara ya rushwa ambapo  Jaji Sammata alisema kuwa kansa hiyo ni kuwanyang'ganya wananchi haki yao hasa matarajio yao ya baadaye ikiwemo maisha bora na maendeleo waliojiwekea, alisema kuwa rushwa  hujenga chuki kwa kuwa huvunja haki na waathirika huchukua sheria mkononi wakiona vyombo husika havijatenda haki.

Jaji Sammata alitoa maoni yake na kusema kuwa ili kuepuka hayo yote lazima elimu zaidi kwa umma itolewe na kushauri vyama vya siasa hasa chama tawala na vyombo vya dola kukemea vitendo hivyo huku akihimiza taasisi za dini zishiriki katika kupinga kampeni hiyo kwa kutoruhusu mapato ya rushwa kutunisha kampeni hizo.

Aidha katika mdahalo huo aliwataka wanasheria nchini kote kuwa mstari wa mbele katika kupinga vitendo hivyo na kuwa waaminifu   bila kujali ukubwa au udogo wa rushwa ambayo zinaathiri maendeleo ya jamii huku akisisitiza watakaokiuka taratibu za kisheria hata wakiwa waandishi wa habari ambao watakutwa na vitendo hivyo katika kazi zao wachukuliwe hatua kali kwa kuwa wao ndio ngao muhimu katika kumulika vitendo hivyo.

Katika mdahalo huo mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya WAJIBU ambaye pia ni  Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu, Ludovick Utouh alisema kiwa taasisi hiyo ni changa na kuanzishwa kwake kulisababishwa na kulegalega kwa uwajibikaji na uadilifu na alihaidi kuendelea kuwafikia walengwa kadri watakavyoweza huku wakiwalenga wanafunzi wa vyuo ambao ndio viongozi watarajiwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad