HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 11, 2019

TEITI KUZIDI KUSIMAMIA MISINGI YAKE YA UWAZI NA UWAJIBIKAJI

*Biteko azitaka kampuni za uchimbaji madini, taasisi za serikali na wachimbaji wadogo kufanya kazi na TEITI

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
TAASISI ya uhamasishaji na uwazi na uwajibikaji katika rasilimali za madini, mafuta na gesi asilia nchini (TEITI) wamefanya warsha iliyowakutanisha wamiliki na makampuni ya madini nchini pamoja na kujadili namna ya kuzidi kukuza sekta hiyo ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa katika pato la taifa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa warsha hiyo Waziri wa Madini Doto Biteko amesema kuwa kamati hiyo inategemewa kwa uwazi, uwajibikaji katika sekta ya uziduaji na amewataka kuzidi kuelimisha wananchi kuhusu kinachoendelea TEITI hasa kuhusiana na machimbo ya madini pamoja na mchango wa kampuni hizo katika jamii.

Biteko amesema kuwa mapato ya wizara hiyo yamepanda kutoka bilioni 190 hadi 200 kwa mwaka hadi kufikia bilioni 390 kwa mwaka na hiyo ni kutokana na usimamizi bora wa Rais Dkt. John Magufuli kwa kusimamia sekta za madini, mafuta na gesi ambazo awali zilikuwa zikilalamikiwa na  wananchi.

Aidha amesema kuwa majina ya makampuni na wamiliki yatawekwa wazi ili watanzania wajue mikataba iliyoingia pamoja na manufaa wanayoyapata huku akiwawataka wamiliki hao kuwa karibu na wananchi kwa kuwa wawazi na wawajibikaji kwani wao ndio mabalozi wao.

Vilevile amempongeza mwenyekiti wa taasisi hiyo Ludovick Utouh pamoja na kamati ya TEITI na kuwataka kushirikiana  wadau hao ambao pia wametakiwa kutekeleza mambo yanayoagizwa na serikali huku akiziagiza kampuni za uchimbaji wa madini,taasisi za Serikali na wachimbaji wadogo wa madini kufanya kazi na TEITI pamoja na kufanya mijadala ya kuboresha sekta hiyo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa TEITI Ludovick Utouh amesema kuwa  malengo ya warsha hiyo ni pamoja na kuelimisha kuhusu shughuli zinazofanywa na TEITI kwa kampuni za madini, mafuta na gesi asilia pamoja na wadau wa sekta ya uziduaji ambapo amesema kuwa TEITI inashirikiana kwa karibu na wizara ya madini katika kuweka wazi mapato yanayopatikana kutoka kwa makampuni ya madini.

Ameeleza kuwa taasisi hiyo itazidi kujenga misingi imara ya uwajibikaji na uwazi hali itakayopelekea kuziba mianya ya rushwa na kuwavuta wawekezaji wengi zaidi. Utouh amesema kuwa uwazi na uwajibikaji katika sekta yoyote ile ndio msingi mkuu katika utekelezaji na ujenzi wa taifa imara.

Warsha hiyo ilienda sambamba na uzinduaji wa Dashbord ya TEIT ambayo taarifa zote zitapatikana huku na hiyo yote ni katika kujenga uwazi na uwajibikaji wa wadau wa sekta hiyo kwa wananchi.
 Waziri wa madini Doto Biteko akizungumza wakati wa uzinduzi wa warsha hiyo ambapo amezitaka kampuni za uchimbaji madini, taasisi za serikali na wachimbaji wadogo kufanya kazi na TEITI, leo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa kamati (TEITI) Ludovick Utouh akizungumza wakati wa uzinduzi wa warsha hiyo ambapo ameeleza misingi ya uwazi na uwajibikaji itazidi kusimamiwa zaidi ili kuzidi kuimarisha sekta hiyo, leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu mtendaji (TEITI) Mariam Mgaya akitoa utambulisho katika warsha hiyo iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Katibu mkuu Wizara ya madini Profesa. Simon Msanjila akizungumza wakati wa uzinduzi wa warsha hiyo ambapo ameshauri kutumia vitu vya ndani huku akieleza kuwa hata mfumo wa TEHAMA wa Dashboard iliyozinduliwa umetengenezwa na vijana hapa nchini, leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa madini Doto Biteko akiwa pamoja na kamati ya TEITI wakati akizindua Dashboard hiyo ambayo imebeba taarifa zote kuhusiana na sekta hiyo, leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad