HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 2, 2019

MAHAKAMA YAWAHUKUMU WAWINDAJI SITA MIAKA 23 JELA KWA KUKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI

Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii

MAHAKAMA ya Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida imewahukumu wawindaji haramu sita kutumikia kifungo cha miaka 23 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa ya nyara za serikali ambazo ni vipande vinne vya meno ya tembo na magamba ya Kakakuona

Aidha Mahakama hiyo imeamuru pikipiki aina ya  Sanlg yenye namba za usajiliT 717 CPD  itaifishwe na kuwa Mali ya serikali.

 Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Stella Kiama ambaye amesema upande wa mashtaka kupitia mashahidi wake sita na vielelezo wameweza kuthibitisha mashtaka pasipo kuacha shaka kuwa washtakiwa walitenda makosa hayo.

Vielelezo ni meno ya tembo, magamba ya kakakuona, pikipiki moja, nyaraka za kuchukulia mali, nyaraka za kuonyesha mwenendo wa vielelezo.
Washtakiwa waliohukumiwa kifungo hicho ni, Aloyce Abiniel, Jonas Chiata, Anton Magomba, Anderson Wami Matayo Rogan na George Joseph.

Akisoma Hukumu hiyo, Hakimu Kiama amesema katika shtaka la kukutwa na vipande vinne vya meno ya Tembo, washtakiwa wote wanahukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 20 gerezani  huku katika shtaka la kukutwa na magamba ya Kakakuona, linalomkabili mshtakiwa wa tano peke yake, amehukumiwa kutimikia kifungo cha miaka 20 gerezani.

 Aidha katika shtaka la tatu, washtakiwa wote hao wamehukumiwa kulipa faini ya sh. 135,542,880.00  na kama watashindwa basi watatumikia kifungo cha miaka mitatu gerezani.

Washtakiwa hao kabla ya kusomewa adhabu walipewa nafasi ya kujitetea ambapo washtakiwa hawakuwa na chochote cha kusema isipokuwa Mshtakiwa wa Chiata kupitia wakili wake alisema yeye ni mkosaji wa kwanza na pia ana familia inayomtegemea mke na watoto na mke wake ni mgonjwa sana.

Katika kesi hiyo upande wa Jamuhuri uliwakilishwa na Wakili wa Serikali, Salimu Msemo, akisaidiana na  Petrida Muta na Tulumanywa Majigo. Na upande wa Utetezi mshtakiwa Chiata alikuwa akitetewa na wakili John Chigongo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad