HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 17 April 2019

LIVIGHA ATIWA HATIANI KWA KOSA LA KUFUJA FEDHA

NA MWAMVUA MWINYI, PWANI

MAHAKAMA ya hakimu mkazi Mkuranga, mkoani Pwani, imemtia hatiani, Sifa Livigha kwa kumpa adhabu ya kifungo cha nje na kutotenda kosa katika kipindi cha miezi sita (conditional discharge) baada ya kufuja fedha kiasi cha sh. milioni mbili.

Aidha mshitakiwa ameamriwa kulipa fedha kiasi cha sh. milioni 2 ,alizokuwa anashitakiwa kuzifuja kinyume na kifungu cha 28 cha sheria ya kuzuiana kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007 .

Hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Mkuranga, Janet Kinyage amemtia hatiani ,Livigha kwa mujibu wa kifungu cha 38(1) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Anasema Livigha alifikishwa mahakamani hapo tarehe 03/05/2018 kwa kosa moja la kufanya ubadhilifu na ufujaji wa fedha hizo kinyume na kifungu cha 28 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Mtuhumiwa alikuwa mwenyekiti wa kitongoji cha Mivule, kijiji cha Mwanambaya wilayani Mkuranga na alifikishwa mahakamani baada ya mwaka 2104 kupokea fedha za ushuru wa kijiji na kuzifuja bila kuziwasilisha ofisi ya kijiji.

Nae kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani, Suzan Raymond alitoa wito kwa wananchi wote popote walipo kuacha kujihusisha na vitendo vya rushwa, badala yake watumie nafasi walizo nazo katika mapambano dhidi ya rushwa.

Vile vile aliwaasa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa kwa njia ya simu ya bure namba 113 (maarufu kwa jina la Longa Nasi) au kwa kufika ofisini pindi wanapobaini uwepo wa vitendo vya rushwa.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad