HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 17 April 2019

CUF YAANZA KUIMARISHA CHAMA KUWEZA KUSHINDA CHAGUZI ZIJAZO MWAKA HUU NA MWAKANI

Na Ahmed Mahmoud Arusha 

Chama cha wananchi. CUF kinajipanga kuhakikisha kinashiriki kikamilifu katika Chaguzi mbali mbali hapa nchini ikiwemo Chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2020 Kwa kuimarisha chama maeneo mbali mbali nchini.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Taifa ulinzi wa chama hicho Masoud wakati alipofanya mahojiano na waandishi wa habari jijini Arusha baada ya kutembelea mikoa ya Dodoma Manyara na Arusha kwenye ziara yake ya kuimarisha chama hicho kwenye mikoa mbali mbali nchini.

Amesema kuwa chama cha wananchi CUF kinajipanga Sawa kuweza kutoa ushindani katika Chaguzi hizo baada ya kutoka katika mgogoro wa viongozi waliondoka na kukimbilia ACT hivyo kimeweka mikakati ya kuimarisha chama hicho kujianda na Chaguzi

"Tumejipanga kukiimarisha chama kushiriki Chaguzi Kwa mafanikio ndio maana tumapita kote kuona chama kinahakikisha kinashinda kwenye Chaguzi zilizo mbele yetu"

Amesema kuwa msingi mkubwa wa chama hicho ni UMOJA Kati ya wanachama na kuimarisha misingi ya chama Kwa kuweza kupata viongozi Bora watakaosaidia jamii kutoka kwenye Lindi la umaskini kuelekea kwa kutekeleza Sera ya utajirisho Kwa watanzania.

Awali akimkaribisha mkurugenzi huyo Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Arusha Omary Selusingo aliwataka viongozi wa chama hicho kuwa kitu kimoja kujenga.chama Kwa misingi ya umoja na mshikamano ili kuweza kufikia lengo.

Amesema kuwa mikakati ya chama hicho ni kuona changamoto mbali mbali zikitatuliwa ikiwemo chama mkoani hapa kuwa na ofisi zake kila wilaya sanjari na vitendeakazi vitakavyosaidia kukiimarisha chama mkoani hapa.

"Chama mkoani hapa kinakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na ofisi ila tumeweka mikakati ya kuhakikisha kata tano ndani ya Jiji la Arusha chama kinashinda Kwa kuanzia na Chaguzi za serikali za mitaa"

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad