WASANII WA KIKE WA KIAFRIKA WAIMBAJI WA MUZIKI WA HIP HOP WAUNGANA KUSHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 8 March 2019

WASANII WA KIKE WA KIAFRIKA WAIMBAJI WA MUZIKI WA HIP HOP WAUNGANA KUSHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKEWakati dunia ikijiandaa kutoa heshima kwa wanawake duniani kote katika Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, chapa ya bia ya kibunifu zaidi Africa, Castle Lite, imeanza safari ya kusherehekea wanawake katika bara zima kwa kuwezesha ushirikiano mkubwa uliopata kutokea wa wasanii wa kike katika muziki wa Hip-Hop kwenye ardhi mama. Lengo lilikuwa ni kuonyesha nguvu pale wanawake wanaposimama pamoja na kuimarisha umoja kwa kupitia muziki, hivyo chapa yetu ilishirikiana na kikundi cha wasanii wakubwa watano (5) wa muziki wa kufoka na kutengeneza tena nyimbo ya msanii malkia wa Hip Hop Queen Latifah iliyokuwa maarufu katika miaka ya 90 ya, U.N.I.T.Y.

 Afrika ya Kusini, Tanzania na Nigeria kwa pamoja waliungana kutengeneza wimbo huu, huku wasanii kama Moozlie (South Africa), Gigi Lamayne (Afrika ya Kusini), Rouge (Afrika ya Kusini), Rossa Ree (Tanzania) na Mz Kizz (Nigeria) wakiwa nyuma ya kipaza sauti. U.N.I.T.Y kutoka Castle Lite ni zaidi tu ya “wimbo mwingine unaoshirikisha wasanii wa kike wa Hip-Hop”, ni wimbo wa kusherekea na wito, sio tu kwa wanawake wote barani kote bali katika kila sehemu ya dunia, kuweka uhai katika nguvu ya wanawake katika muungano.

Wasanii watano kwa wakati mmoja waliimba U.N.I.T.Y mubashara asubuhi ya leo katika Instagram; Jambo la kwanza kabisa kufanyika kwa Castle Lite na kwa bara zima la Afrika kwa ujumla. Akizungumza baada ya onyesho (livestream), Mkurugenzi wa chapa ya Castle Lite Silke Bucker alisema: “Msingi wetu kama Castle Lite kila siku umekuwa ni kuvuka mipaka kwa kutumia ubunifu, na ili kuweka kumbukumbu katika siku hii ya kipekee, hakukuwa na njia nzuri zaidi kwetu kuunganisha wanawake zaidi bali kwa kutumia jambo ambalo kiukweli tunalolipenda – muziki.”

“Mshikamano wa kimuziki katika bara zima ulifanya jambo hili la wasanii kuja pamoja kufanya wimbo pamoja na chapa yetu kuwa la asili, na Castle Lite imebahatika imeamua kuwaweka wanawake katika hip-hop mbele. Leo sote tunasherekea nguvu ya wanawake katika UMOJA na

tunazidi kung’ara zaidi na kwa fahari kubwa tukisherekea na wanawake wote duniani kote katika siku hii ya kipekee na ya kimataifa,” Bucker alimalizia kusema. “Ni hesima kubwa sana kuwa sehemu ya harakati ambazo sio tu kwamba zinasherekea na wanawake, lakini zinachochea

UMOJA kwa kupitia muziki. Muziki una uwezo wa kuunganisha watu kutoka katika mazingira tofauti, na ni kwa kupitia suala hili tuliweza kufanya jambo la tofauti kwa namna yetu ya kipekee ili kutengeneza wimbo huu mzuri ukiwa na ujumbe wenye nguvu.” Moozlie Aliongeza Mwaka jana, chapa hii yenye bia ya baridi ilivunja mipaka ya kimuziki ilipokuwa mwenyeji wa onyesho la kwanza na la kipekee la wasanii wa kike wa Hip Hop lililoitwa Hip Hop Herstory, ambalo lilijikita katika kuonyesha nafasi ya wanawake katika mabadiliko ya Hip Hop.

Onyesho la Hip Hop Herstory kutoka Castle Lite lilifanikiwa na baada ya kujifunza kutokana na hilo ilimaanisha kwamba ushirikiano wa U.N.I.T.Y sio tu kwamba ulikuwa na mantiki lakini pia ni hatua kwenda mbele katika kuonyesha na kutoa heshima kwa vipaji na michango ya wasanii wetu wenyewe kutoka Afrika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad