HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 8 March 2019

KIFO CHA KIBONDE NI PENGO KUBWA KWA TAIFA-MAJALIWA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Mtangazaji wa Clouds FM, Efraim Kibonde wakati alipokwenda nyumbani kwao marehemu, Mbezi Beach jijini Dar es salaam kutoa pole kwa familia, Machi 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Samson Job Kibonde ambaye ni baba mzazi wa Mtangazaji wa Clouds FM, Ephrim Kibonde wakati alipokwenda nyumbani kwao marehemu, Mbezi Beach jijini Dar es salaam kutoa pole kwa familia, Machi 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimfariji Hilda Samson Kibonde ambaye ni mama mzazi wa Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde wakati alipokwenda nyumbani kwao  marehemu, Mbezi Beach jijini Dar es salaam, kutoa pole kwa familia, Machi 8, 2019. Katikati ni baba mzazi wa marehemu, Samson  Job Kibonde. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Samson Job Kibonde ambaye ni baba mzazi wa Mtangazaji wa Cloud FM, Ephrim Kibonde wakati alipokwenda nyumbani kwao marehemu, Mbezi Beach jijini Dar es salaam kutoa pole kwa familia, Machi 8, 2019. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Clouds Media, Joseph Kusaga.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema kifo cha aliyekuwa Mtangazaji Muandamizi wa kituo cha redio cha Clouds, Ephraim Kibonde ni pengo kubwa kwa Taifa, Clouds Media Group na tasnia ya habari kwa ujumla.

Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Machi 8, 2019) alipokwenda kuhani msiba wa Mtangazaji Muandamizi kituo cha redio Clouds, Kibonde kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mbezi Beach Dar es Salaam.Kibonde alifariki dunia jana alfajiri Machi 7, 2019 jijini Mwanza.

“Msiba huu umetushtua sana na ni tukio ambalo hatukulitarajia ila ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Hivi karibuni sote tulimshuhudia akiongoza ratiba ya kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba na alienda hadi Kagera kumzika.”

Waziri Mkuu amesema marehemuKibonde enzi za uhai wake ameshirikiana vizuri na Serikali katika shughuli mbalimbali, hivyo amewaomba wananchi waendelee kushikamana na kuifariji familia. “Tumuombee marehemu apumzike kwa amani.

Kadhalika, Waziri Mkuu ametoa wito kwa wazazi, watoto wa marehemu pamoja na wananchi kwa ujumla waendelee kuwa na subira na watulivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad