HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 19, 2019

WANAWAKE KUPATA FURSA KATIKA MASUALA YA KIUCHUMI KUPITIA SEKTA BINAFSI

* Washauriwa kutumia fursa za kiuchumi na biashara  zinazojitokeza 

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii
JUKWAA la nane la Canada linalofanyika nchini kila mwaka limeadhimishwa leo jijini Dar es Salaam huku likijadili ushiriki wa wanawake katika sekta binafsi na namna zinavyochangia maendeleo yao pamoja na changamoto wanazokumbana nazo.

Akifungua jukwaa hilo ambalo limeandaliwa na mtandao wa Haki rasilimali, ubalozi wa Canada, taasisi ya sekta binafsi nchini (TPFS)na Policy Forum Tanzania, balozi wa Canada nchini Pamela O'Donnel amewashukuru washiriki wa  jukwaa hilo ambalo litanyanyua wanawake wengi katika kufikia malengo yao, amesema kuwa jukwaa hilo pia litaweka mazingira bora ya biashara na uchumi kwa wanawake.

Amesema kuwa Canada itaendelea kushiriki katika masuala ya kuwainua wanawake ikiwa ni pamoja na masuala ya usawa wa kijinsia, pia ameeleza kuwa wataendelea kushauri na kuhakikisha haki za mabinti na wanawake zinakuwa na thamani.

Akimwakilisha Mkurugenzi mkuu wa kituo cha uwekezaji nchini (TIC,) Mkurugenzi wa idara ya Uhamasishaji kutoka kituo cha uwekezaji nchini John Mnali amesema kuwa semina hiyo italeta matunda bora kwa wanawake hasa katika fursa za uwekezaji na upatikanaji wa mikopo na masoko.

Amesema kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo wanawake katika sekta binafsi ni kutopata fursa za ushiriki wa kutosha pamoja na uchache wa mitaji na amezishauri taasisi za kiserikali na binafsi kuzidi kuongeza na kuendeleza ushiriki wao kwa wanawake katika fursa mbalimbali.

Pia Mkurugenzi wa huduma kwa wanachama kutoka taasisi za sekta binafsi nchini (TPSF) Louis Accaro amesema kuwa lazima wanawake wapate nafasi katika biashara  na kupata huduma stahili kutoka kwa watoa huduma na wao kama TPSF watasukuma na  kuhakikisha  wanawake wanashiriki katika shughuli za kiuchumi na uzinduaji.

Amesema kuwa katika sekta ya madini kuna wachimbaji wadogowadogo wapatao milioni 6 huku akihoji ni idadi ngapi ya wanawake wanashirikishwa.

Accaro amesema kuwa mabaraza ya taifa ya uchumi yaliyoko katika Mikoa na Wilaya zote nchini yatumike vyema katika kuweka mazingira bora ya biashara hasa kwa wanawake.

Vilevile  Mratibu wa mtandao wa haki rasilimali nchini  Rachel Chagonja amesema kuwa sasa ni wakati wa kujadili nafasi ya mwanamke katika manufaa ya mnyororo wa thamani katika mambo yatakayowapeleka mbele yakiwemo masuala ya mafuta, gesi pamoja na madini.

Rachel amesema  kuwa sekta  uzinduaji inaonekana kuwa ngumu kutokana na changamoto za uendeshaji wake ila amewataka wanawake kuwekeza nguvu zao katika shuguli hizo na kuwashauri  kutumia fursa hizo na kuonesha ujuzi wao katika sekta hizo za madini, mafuta na gesi katika kujenga uchumi wao na taifa kwa ujumla.
 Balozi wa Canada nchini Tanzania, Pamela O'Donell akizungumza na wadau wa sekta binafsi katika jukwaa la Canada la miaka nane ambalo limejadili ushiriki wa wanawake katika sekta binafsi, ambazo ni pamoja na Mafuta, Madini, gesi,  lililoandaliwa na TPSF Policy Forum, ubalozi wa Canada nchini Tanzania pamoja na Haki Rasilimali.
Washiriki wa mjadala wa Jukwaa la Canada la miaka nane ambalo limejadili ushiriki wa wanawake katika sekta binafsi, ambazo ni Mafuta, Madini, gesi na ICT, wakisikiliza Hotuba ya mgeni rasmi, ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Uhamasishaji na uwekezaji kutoka kituo cha uwekezaji nchini, John Mnali hayupo pichani kwa niaba ya  Mkurugenzi wa kituo cha hicho cha uwekezaji.
 Mkurugenzi wa Idara ya Uhamasishaji na uwekezaji kutoka kituo cha uwekezaji nchini, John Mnali akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya  Jukwaa hilo na kuahidi wanawake kupatiwa fursa za uwekezaji ikiwa ni pamoja na kupatiwa mikopo na amezitaka taasisi Mbali Mbali kuongeza ushiriki wa wanawake katika njanja Mbali Mbali  za kiuchumi.
 Mratibu wa Mtandao wa haki Rasilimali Rachael Chagonja akiwaeleza  wanahabari namna mwanamke anavyoweza kushiriki katika shughuli yoyote ya kiuchumi Inayoonekana kuwa ngumu katika kuleta maendeleo. Aidha amewashauri wanawake kutumia fursa zinazojitokeza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad