HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 12, 2019

WANANCHI WAJITOLEA KUWEKA ALAMA ZA BARABARANI

Na Ahmed Mahmoud, Arusha.
Wananchi  wa kata ya  Lemara  eneo la Nanenane  jijini Arusha wameamua kujitolea kwa hali na mali kuweka  alama za vivuko  viwili  vya waenda kwa miguu katika barabara inayoingia katikati ya jiji kwenye eneo linalodaiwa kutokea  ajali za mara kwa mara  na kusababisha watu wasiyo na hatia kupoteza maisha .

Wanahabari walifika kwenye  eneo la nanenane na kushuhudia  wakazi wa eneo hilo wakichangishana fedha kwa ajili na kuweka alama hizo huku mafundi wakiendelea  na kazi ya kuweka alama hizo ambazo zinatajwa kua ni suluhisho la kuzuia  ajali kutokea katika  eneo hilo.

Wakazi wa kata hiyo wakizungumzia hatua waliochukua ya kujitolea kwa michango yao wakishirikiana na diwani wao nibaada ya eneo hilo kukidhiri ajali za mara kwa mara ambazo wakati mwingine zinaepukika.

Alfredy Maulid na Pascal Silvery ni  wakazi wa kata ya  lemara walisema upatikanaji wa kivuko hicho  ni mkombozi mkubwa  hasa watoto wa shule kuvuka kwa amani kwakua kipindi cha nyuma hali ilikua mbaya ya watu kupoteza maisha kwa kugongwa na magari.

Pascal alisema kuwa wanaamini kuwepo kwa alama hizo kutasaidia wanaovuka waweze kuvuka salama hususan wanafunzi ambao hupata adha kubwa wanapotaka kuvuka barabara.

Diwani wa kata ya Lemara  Profesa   Raymond Mosha  alisema kuwa    ameungana na  wananchi  kutokana na  umuhimu wa eneo hilo  hawezi kuvumilia kuona watu wakiumia wakati wananchi wanaweza kujitoa na kufanikisha  jambo hilo .

“Ushirikiano kati ya Wananchi na Viongozi wao umeweza kufanikisha jambo hili muhimu ,tayari  tulishatoa taarifa uongozi wa Jiji umetoa ridhaa kwa wananchi kufanya jambo hili hivyo lina Baraka zote za jiji” Alisema Profesa Mosha

Dereva wa magari Johnson Mlay    alisema  hatua  iliyofanywa na wananchi  itawasaidia   kufuata sheria  ili kuepusha ajali zisizo za lazima
Mafundi wakiweka alama za vivuko  barabarani katika eneo la Nane nane  jijini Arusha baada ya Wananchi  kata ya Lemara kuchangia zoezi hilo ambalo limefanyika kwa kushirikiana na Wataalamu kutoka Jiji la Arusha ili kuzuia ajali za barabarani hususan kwa wanaopita kwa miguu. Picha na Mahmoud Ahmad Arusha.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad