HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 12, 2019

HOTEL YA ILBORU SAFARI YATEKETEA KWA MOTO

Na Ahmed Mahmoud,Arusha
Hoteli ya Kitalii ya Ilboru Safari Lodge inayomilikiwa na kanali Mstaafu wa Jwtz Mika Metil iliyopo Ilboru wilaya ya Arumeru, Mkoani hapa imeteketea kwa Moto uliozuka Mapema Leo na kuteketeza vitu vyote vilivyokuwemo ndani ikiwemo kisanduku(Selfu) cha kuhifadhia fedha kinachodaiwa kuhifadhi mamilioni ya fedha.

Tukio hilo limetokea majira ya Saa 20.30 asubuhi huku chanzo cha Moto huo kikiwa bado hakijajulikana na taarifa za awali zinadai ni kutokana na hitilafu ya umeme. Moto huo pia umetetekeza Nyumba mbili za kulala wageni ikiwemo ofisi ya Mkurugenzi wa hotel hiyo ambaye ni Raia wa Kigeni.

Akizungumzia tukio hilo ,Kanali Metil pamoja na  kusikitishwa na tukio hilo Alisema kwa sasa hamiliki hotel hiyo kwani ameikodisha miaka 10 iliyopita kwa mwekezaji ambaye ni raia wa Kigeni.

Kwa upande wake meneja wa hotel hiyo,Eddy Jack amesema kuwa moto huo ulizuka leo majira ya asubuhi ambapo waliwasiliana na jeshi la zima moto na wokozi ambao walifika eneo la tukio na kukuta sehemu kubwa ya mali zimeteketea kiasi cha kutookoa chochote.

Hata hivyo alieleza kuwa jeshi la zima moto na uokozi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na kampuni binafsi ya ulinzi walifanikiwa kuimarisha ulinzi na kufanikiwa kuzima moto huo ingawa ulishateketeza sehemu kubwa samani za ndani na majengo.

Hata hivyo utata umeibuka katika tukio hilo la kuungua kwa hotel mara baada ya kuibuka taarifa zinazodai kufanyika hujuma juu ya tukio hilo. Tukio hilo limeibua utata mkubwa Mara baada ya Mamilioni ya Fedha zikiwemo za kigeni zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye kisanduku  'Selfu'kutoonekana.

Licha ya kisanduki hicho kuungua na Moto lakini ilipofunguliwa haikukutwa na kiasi chochote cha fedha huku raia huyo wa Kigeni Anneliese Metil ambaye anayeendesha hotel hiyo kwa sasa, akiangua kilio akidai kuhujumiwa na ataeleza kila kitu kilichofanyika Mara atakapokuwa sawa kiakili.

Ameeleza kuwa wao kama wafanyakazi hawana mamlaka ya kuingia ndani hivyo kutoweza kusema chochote kama kiasi kilichopotea au thamani ya Mali Zaidi kueleza tukio na uongozi utatoa taarifa kwenu baada ya kutoa tathmini ya Mali na majengo vilivyoteketea.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha,Jonathan Shanna alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa thamani halisi ya Mali zilizoteketea hakijajulikana na Polisi wanaendelea na uchunguzi.

Alifafanua kuwa katika tukio hilo nyumba mbili za kuishi zimeteketea kabisa huku chanzo cha ajali hiyo kikiwa bado hakijulikani na kwamba uchunguzi unaendelea na hakuna aliyejeruhiwa na wala hakuna anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo.
 Sehemu ya vyumba vya kulala wageni kwenye hotel ya Iboru Safari lodge baada ya kuzimwa Moto vikiwa vimeteketea. Picha zote na Mahmoud Ahmad Arusha. 
 Jengo la hotel ya Iboru Safari lodge likiwa limeteketa baada ya kuzuka Kwa Moto majira ya saa mbili na nusu asubuhi leo wilayani Arumeru .
 Sehemu ya mabaki ya Kishubaka cha kuhifadhia fedha selfu kikiwa kitupu mara baada ya kufunguliwa na kuzua taharuki Kwa mmiliki wa hotel hiyo Raia wa kigeni Anneslies Metil.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad