HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 1, 2019

TAMASHA LA KIBIASHARA LA KIMATAIFA LAFANYIKA GÖTEBORG SWEDEN 2019

TAMASHA  la Siku ya biashara la kimataifa limefanyika katika mji wa Goteborg Sweden magharibi ikiwa ni katika kuendelea kuwasaidia washiriki na wamiliki wa kampuni kufahamu mwenendo wa biashara na mkakati wa mauzo ndani na nje ya Sweden pamoja na Ulaya.

Mambo muhimu  yaliyojadiliwa katika mkutano huo  ni pamoja na changamoto Katika ulimwengu wa biashara katika dunia ya leo na kimataifa.

Mkutano huo ulikua ni wakati muafaka wa kukutana na wamiliki na viongozi mbali mbali wa makampuni kutoka pembe mbali mbali za dunia na makampuni mengine ya kuuza nje na maslahi Sawa kwa wote. Zaidi ya kampuni 190 zimehudhuria kutoka kila nyanja ya biashara halikadharika benki kubwa zikiwemo Swedbank na Nordea waliovutiwa sana na taswira ya Tanzania kwasasa.

 Balozi Dr Willibrod Peter Slaa akiwa na mkalimani nguli mswedishi Denis Nystrom aka Juma alieishi Tanzania kwa miaka 17 alimsaidia Mh balozi kutafsiri toka lugha ya kiswedishi kwenda kiswahili fasaha
 Balozi Slaa akizungumza na Mr Livio Benedetto afisa uhusiano mambo ya nje toka mji wa Trollhattan aliesimama Katika na kulia ni mkuu wa mambo ya nje kutoka Export center west of Sweden region Mr Olle Jonäng.
Team Tanzania waliwakilisha vyema chini ya uongozi wa Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dk Willibrod Slaa , kutoka kushoto ni Chef Issa, Afisa ubalozi Mr Juma Ndwatta, Mh balozi Slaa, mjasilia Mali Ms Nimco Kapande, Mkalimani Mr Denis Nystrom aka Juma, afisa ubalozi Bi Joyce Malipula na afisa ubalozi Ms Agnes Mwaiselage.
 Mjalisimali Katika idara ya chakula na lishe Chef Issa pia alishiriki kuwakilisha upande wa wafanyabiashara upande wa Tanzania
 Maafisa wa ubalozi waliohudhulia kutoka kulia kwenda kushoto ni afisa Juma Ndwatta, Joyce Malipula na Agnes Mwaiselage na wa mwisho ni Chef Issa.
 Panel discussion ikiendelea na hayo hapo juu ndio majina ya watoa Mada
Balozi Slaa alihudhuria pia seminar maalumu kwajili ya Norway 🇳🇴 wa kumzungumzia fursa na changamoto za Uwekezaji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad