HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 22, 2019

RAIS MAGUFULI KUWA MGENI RASMI SHEREHE ZA MEI MOSI MBEYA

Na Emanuel Madafa, Mbeya 

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Albert Chalamila amesema Rais Dkt Magufuli amekubali kuwa mgeni rasmi katika sherehe za Meimosi  nchini ambazo kitaifa zinatarajiwa kufanyika Mkoani Mbeya.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya ametoa kauli hiyo jijini Mbeya katika kikao cha kwanza cha Maandalizi kwa ajili ya sherehe hizo za wiku ya wafanyakazi Nnhini ambacho kimehudhuliwa na viongozi wa shirikisho la vyama vya vya wafanyakazi Nchini TUKTA.

Chalamila amesema kuanzia tarehe moja watakuwa na ugeni wa Rais Dkt Magufuli hivyo wanacho subiri kwa sasa ni taratibu na taarifa Kutoka kwenye Ofisi yake ambayo itaweka bayana ujio wa Rais Magufuli katika sherehe hizo za Mei Mosi Mkoani hapa .

“Rais amekubali kuwa mgeni rasmi kwahiyo tunatarajja kwamba kuanzia tarehe moja tutakuwa nae ,ni lini atafika mkoani mbeya hii tunasubiri taarifa na taratibu kutoka katika ofisi yake na tutapewa kwa maandishi kwamba sasa Rais magufuli anakuja lini na wakati gani “RC Chalamila.

Aidha kuhusu ushiriki wa vyama vya kisiasa katika sherehe hizo za Mei Mosi Mkuu huyo wa Mkoa amesema wanachokitaka nikuona sherehe hizo haziegemei katika upande mmoja wa chama cha kisiasa kwani tukio hilo ni kubwa na linabeba  taswira ya watu mbalimbali wakiwemo Viongozi wa kitaifa wa serikali na vyama .

“Vyama vya kisiasa vinavyama  vyao hivyo vitashiriki  vizuri kabisa tunachokitaka sisi nikwamba hatupendi tukio hilo lionekane linaegemea upande mmoja wa chama  cha kisiasa,bali ni tukio ambalo litakuwa na malengo ,hisia na matarajio ya kitaifa ambapo wageni mbalimbali watakuwa hapa.”Amesema Chalamila.

Wakati huo Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa huo kujitokeza kwa wingi katika sherehe hizo nakwamba serikali haita zuia mtu yeyote kuandika bango lolote ili mradi liwe limeandika kitu che haki .

Sherehe hizo za Mei Mosi zilifanyika Mkoani hapa 2013 na kuhudhuliwa na Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad