HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 13 March 2019

MKUTANO WA AFRICA NOW WAFUNGULIWA JIJINI KAMPALA

Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Africa Now Summit 2019 ambapo viongozi wa Afrika wanakutana kujadili masuala mbalimbali ya utengamano katika kuleta maendeleo endelevu barani Afrika ambapo Tanzania imewakilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye mkutano wa Africa Now Summit 2019 uliofanyika kwenye hoteli ya Commonwealth Resort, Munyonyo jijini Kampala, Uganda. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali walihoudhuria mkutano wa Africa Now Summit 2019 uliofanyika kwenye hoteli ya Commonwealth Resort, Munyonyo jijini Kampala, Uganda. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Mkutano ukiendelea
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akiwa na mwenyeji wa Mkutano wa Africa Now Summit 2019 Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni pamoja na Rais wa Somalia Mhe. Mohamed Abdullahi Mohamed (kulia) wakati wakielekea kwenye ukumbi wa mkutano katika hoteli ya Commonwealth Resort, Munyonyo jijini Kampala Uganda. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad