KAMATI ya kitaifa ya mradi mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) imekutana jijini Dar es salaam kupitia pamoja na mambo mengine ratiba ya utekelezaji wa mradi huo.
Mradi huo ambao unajulikana kama The Better Education for Africa's Rise, (BEAR) unaendeshwa pia katika nchi za Madagascar, Ethiopia, Uganda na Kenya na ni sehemu ya mradi wa kimataifa wa elimu maarufu kama Education 2030 Agenda , moja ya malengo ya maendeleo endelevu ya kimataifa, lengo namba nne, na unafadhiliwa na Korea kusini kwa dola za Marekani milioni 10.
Akizungumza Mkuu wa Kitengo cha Elimu katika Shirika la UNESCO nchini, Faith Shayo alisema kwamba mradi huo unaotarajiwa kukamilika 2021 umelenga kuboresha utaalamu na kuwezesha vijana kuajiriwa au kujiajiri wenyewe kwa kuangalia fursa zilizopo kwa kadri ya mahitaji ya nchi.
Mradi huo ambao sasa unaingia katika awamu ya pili,na hivyo kujulikana kama BEAR ll ulianza mwaka 2017 na unatarajiwa kutekelezwa hadi 2021, kazi kubwa ikiwa ni kuwezesha vijana kupata ajira zenye staha na pia kujenga uwezo wa kujiajiri kwa vijana kwa kuboresha mifumo na ufundishaji wa elimu ya ufundi stadi.
Alisema nchini Ethiopia, mradi huu umejikita zaidi katika sekta ya uchakataji mazao ya kilimo; Kenya ipo uhifadhi wa mazingira, utengenezaji wa nafasi za kazi za kutunza mazingira; Madagascar ipo kwenye viwanda vya nguo; Uganda imejikita katika menejimenti ya mazao baada ya kuvunwa na uchakataji wa bidhaa za chakula zinazotokana na kilimo wakati nchini Tanzania imejikita katika biashara za mazao ya kilimo na ubunifu.
“Tunatarajia baada ya kukamilika kwa mradi huu kutakuwepo na maendeleo makubwa katika mifumo ya elimu na ufundishaji wa elimu ya ufundi stadi nchini Tanzania,” alisema Shayo wakati akiwasilisha mpango kazi unaotakiwa kufuatwa katika kikao hicho cha kitaifa mwishoni mwa wiki.
Alisema kwamba BEAR II inatekelezwa kwa kuzingatia fundisho lililopatikana kwenye awamu ya kwanza iliyoanza 2011-2016 ambayo ilisaidia kunoa mifumo ya ufundi stadi na ufundishaji wake katika nchi 5 za Jumuiya ya Uchumi Kusini mwa Afrika (SADC)  za Botswana, DR Congo, Malawi, Namibia, na Zambia.
BEAR II ambayo inajengwa  kwa kuzingatia vipaumbele vya kila taifa, inaingilia maeneo matatu ili kufanya mafunzo ya ufundi kuwa na maana zaidi kwa kuzingatia mahitaji ya kiuchumi na soko; kuboresha zaidi programu zinazoambatana na elimu hiyo na pia kuboresha uelewa na matamanio ya elimu ya ufundi miongoni mwa vijana.
Mradi wa BEAR kwa kila nchi unafanywa kwa ushirikiano kati ya wadau mbalimbali wa elimu, wizara ya elimu na serikali za nchi husika.
Imeelezwa kuwa kazi kubwa ya UNESCO katika mradi huo ni ya menejimenti, ufuatiliaji na ufanyaji wa tathmini na serikali ya Korea yenyewe itatengeneza mfumo wa ufuatiliaji na kufadhili utekelezaji wake.
 Ofisa
 wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO),
 Jennifer Kotta akitambulisha meza kuu wakati wa kikao cha kamati ya 
kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa kuboresha 
elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika 
ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia
 Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) 
uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es 
Salaam.
 Mkuu
 wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
 na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos akitoa neno la 
ukaribisho wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya 
utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) 
kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na 
binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa 
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa
 wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu
 Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo.
 Mwenyekiti
 wa kikao ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na 
Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo (wa pili kushoto) akibariki kuanza kwa 
kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi 
huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la 
kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi 
unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la 
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki 
Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni 
Naibu Balozi wa Ubalozi wa Korea Kusini nchini, Jiin An, Naibu Katibu 
Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Abdulla Mzee Abdulla 
(wa pili kulia) pamoja na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la 
Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. 
Tirso Dos Santos (kushoto).
 Mkuu
 wa Kitengo cha Elimu katika Shirika la UNESCO nchini, Faith Shayo 
akifafanua jambo wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia 
ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi 
(BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali 
sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja
 wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni
 mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi
 wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi wa Wizara ya Elimu, 
Sayansi, Teknolojia Dk. Noel Mbonde akiwasilisha mpango kazi wa mradi wa
 BEAR II wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya 
utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) 
kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na 
binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa 
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa
 wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Naibu
 Balozi wa Ubalozi wa Korea Kusini nchini, Jiin An akishiriki kwenye 
majadiliano na makubaliano kuhusu mpango kazi wa mradi wa BEAR II wakati
 wa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa 
mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la 
kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi 
unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la 
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki 
Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu 
Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Abdulla Mzee Abdulla
 Naibu
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Abdulla Mzee 
Abdulla akiwasilisha maoni kwenye majadiliano na makubaliano kuhusu 
mpango kazi wa mradi wa BEAR II wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa 
cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu
 ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira 
mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia 
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) 
uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es 
Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na 
Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo na kulia ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi
 wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) 
nchini, Bw. Tirso Dos Santos.
 Mwenyekiti
 wa kikao ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na 
Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo (katikati) akiendesha majadiliano na 
makubaliano kuhusu mpango kazi wa mradi wa BEAR II wakati wa kikao cha 
kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa 
wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo 
vijana katika ajira mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea 
Kusini kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na 
Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea 
Courtyard jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya 
Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Abdulla Mzee Abdulla na kulia ni 
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, 
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos
 Ofisa
 Mwandamizi Elimu, kitengo cha Elimu ya Ufundi Stadi, Wizara ya Elimu, 
Sayansi na Teknolojia, Bi. Fides Lubuva akiwapitisha wajumbe kwenye 
bajeti wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya 
utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) 
kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na 
binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa 
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa
 wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Kaimu
 Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Tume ya Taifa ya Unesco (UNESCO-NATCOM), 
Francis Msungu akishiriki kwenye majadiliano na makubaliano kuhusu 
mpango kazi wa mradi wa BEAR II wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa 
cha kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu
 ya ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira 
mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia 
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) 
uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es 
Salaam.
 Sehemu
 ya wajumbe wa kikao cha kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya 
utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) 
kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na 
binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa 
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa
 wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Mmoja
 wa wajumbe akichangia maoni wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa cha 
kupitia ratiba ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya 
ufundi (BEAR II) kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira 
mbalimbali sokoni na binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia 
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) 
uliofanyika mwishoni mwa wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es 
Salaam.
Katibu
 Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo 
akiwa kwenye picha ya pamoja na kamati ya kitaifa cha kupitia ratiba ya 
utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kuboresha elimu ya ufundi (BEAR II) 
kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana katika ajira mbalimbali sokoni na 
binafsi unaofadhiliwa na Korea Kusini kupitia Shirika la Umoja wa 
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliofanyika mwishoni mwa
 wiki Hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.

No comments:
Post a Comment