HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 1, 2019

HAKUNA TENA NAFASI YA KUFANYA MAKOSA KATIKA MANUNUZI-DKT JINGU

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amewaonya viongozi na baadhi ya watumishi wa Wizara yake kuwa hakuna nafasi tena ya kufanya makosa katika utendaji kazi kwa kuwa tayari wana ufahamu mkubwa wa sheria ya manunuzi.

Alisema hayo wakati hotuba yake kwa watumishi hao wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu kuhusu sheria ya manunuzi nakuongeza kuwa wanatakiwa kusoma zaidi sheria hiyo baada ya kuwa wamepata mwanga wa kutosha kutokana na mafunzo hayo.

Aidha Kiongozi huyo aliongeza kuwa kutokana na kukosa ufahamu wa sheria ya manunuzi baadhi ya watumishi walikuwa wanafanya makosa ya kimajukumu kwa kutekeleza majukumu ya watu wengine na kuonya kuwa inabidi wajilizishe na sheria ili kuepuka mwingiliano katika majukumu yao.

‘’Baada ya kupitia mafunzo ya majukumu ya kila mtu kisheria ni matumaini yangu kuwa hakutakuwa nafasi tena ya kufanya makosa kwa kufanya maamuzi yanayokiuka sheria na kujikuta unatekeleza majukumu ya mtu mwingine kama vile kutekeleza majukumu ya Katibu Mkuu wakati wewe huna mamulaka hayo.’’ Aliongeza Dkt. Jingu.

Aidha amewataka viongozi na watumishi hao kuepuka na makosa ya rushwa akionya kuwa makosa hayo ni makubwa na yanashughulikiwa na vyombo husika akiwataka kujiepusha nayo kwani mtu akibainika atapata misukomisuko mikubwa jambo ambalo linaepukika.

Aidha amechukua fursa hiyo kuwataka wafanyakazi wote kuacha kufanya kwa mazoea na kuwataka kuwa wabunifu katika maweneo yao ya kazi na katika Jamii zinazowazunguka ili jamii husika iweze kufaidika na kuwepo kwa taasisi mahali hapo.

Amewaagiza Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kuhakikisha  wanakuwa na ubunifu na pia kutumia rasilimali zilizopo katika maeneo yanayozunguka vyuo ili wananchi wanaoishi jilani na vyuo hivyo waweze kunufaika na uwepo wa chuo katika maeneo yao.

‘’Kuweni wabunifu achana na kufanya kazi kwa mazoea ili wanajamii wanao wazunguka waweze kunufaika na uwepo wa chuo katika maeneo yao mfano Chuo cha Rundenga kwasasa kinasindika zao la karoti na bidhaa zitokanazo na uwekezaji huo zinauzwa kwa jamii jambo hili ni zuri sana.’’ Aliongeza Dkt. Jingu. 

Mafunzo hayo kwa viongozi wa Wizara, Viongozi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii pamoja na maafisa wa serikali yanahusu sheria ya Manunuzi ya Serikari ya Mwaka 2011 na mabadiliko ya kanuni zake ya mwaka 2013 kama ilivyorekebishwa mwaka 2016.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akiongea na viongozi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii pamoja na Wakurugenzi wa Wizara wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu ya sheria ya manunuzi.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya manunuzi ya Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akiongea jambo wakati wa kuhitimisha mafunzo ya siku tatu kwa viongozi wa wizara na Wakuu Vyuo vya Maendeleo ya Jamii jana Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Manunuzi ya Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Martha Chuma akiongea jambo wakati wa kuhitimisha mafunzo ya siku tatu kwa viongozi wa wizara na Wakuu Vyuo vya Maendeleo ya Jamii jana Jijini Dodoma.
 Baadhi ya Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii pamoja na Wakurugenzi wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii wakifuatilia jambo wakati wa kuhitimisha mafunzo ya siku tatu kwa viongozi wa wizara na Wakuu Vyuo vya Maendeleo ya Jamii jana Jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad