HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 11, 2019

CHECHE ATAMBA USHINDI WA AZAM NI KUCHEZA NA AKILI ZA WACHEZAJI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KOCHA wa muda wa Azam FC, Idd Nassor Cheche, amesema kuwa timu hiyo ina matokeo mazuri hivi sasa kutokana na kufanikiwa kucheza na akili za wachezaji.

Azam wamefaniiwa kupata ushindi wa goli 6-1  dhidi ya  JKT Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.


Ameyasema hayo baada ya kufanikiwa kuondoka na ushindi mnono wa pili wa mabao zaidi ya mabao matano kuwahi kuupata kwenye ligi hiyo, awali iliwahi kuipiga Villa Squad mabao 6-2 msimu wa 2008/2009.



Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Cheche anayesaidiana na Meja Mstaafu, Abdul Mingange, ameuambia mtandao rasmi wa klabA alisema kama ukishindwa kucheza na akili za wachezaji basi unaweza kuwa na wachezaji wazuri lakini ukashindwa kuwatumia.

“Unaweza ukaja na mazoezi mengi lakini ukaja na vitu vingi lakini bila kucheza na akili zao mafanikio yanakuwa ni magumu,” alisema

Akizungumzia ushindi huo mnono, licha ya ubora wa timu ya JKT Tanzania, ikiwa ngumu kufungika, Cheche alisema kuwa: “Mimi nasema kwenye mpira linawezekana, kama Brazil waliweza kufungwa goli saba kwao, kwanini JKT wasifungwe goli sita?,” alihoji Cheche.

Huo ni ushindi wa tatu mfululizo kwa kikosi hicho kikiwa chini ya makocha hao wa muda, awali ilitangulia kuzichapa Rhino Rangers (3-0) kwenye kombe la FA na kutinga hatua ya robo fainali kabla ya kuinyuka African Lyon 3-1 kwenye mchezo wa ligi.

Mara baada ya mchezo huo kikosi cha Azam FC, kinatarajia kurejea mazoezini leo Jumatatu, kuanza maandalizi ya kuikabili Singida United, utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex, Machi 16  huu saa 1.00 usiku. 

Mabao ya Azam  yamewekwa kimiani na mshambuliaji Donald Ngoma, aliyetupia mawili, nahodha Agrey Moris, Obrey Chirwa, Mudathir Yahya na Danny Lyanga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad