BancABC
 kupitia Huduma  ya Mkopo Rahisi imejidhatiti kuhakikisha inainua na 
kuendeleza mazingira ya elimu katika wilaya ambazo benki hiyo inafanya 
shughuli zake kupitia miradi yake ya kusaidia jamii inayowazunguka. 
Akizungumza katika hafla hiyo fupi Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi Bw.
 Emmanuel Nzutu alisema  wanaunga mkono juhudi za serikali  kutoa elimu 
bure kwa kila Mtanzania kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne.
" Hivyo leo sisi kama Bancabc tunatoa msaada wa mabati 200 kwa wilaya ya Kilindi, na msaada huu tunaukabidhi hapa kwa Mkuu wa Wilaya Mhe. Sauda Salum Mtondoo.”
" Hivyo leo sisi kama Bancabc tunatoa msaada wa mabati 200 kwa wilaya ya Kilindi, na msaada huu tunaukabidhi hapa kwa Mkuu wa Wilaya Mhe. Sauda Salum Mtondoo.”
Alisema
 BancABC  inaamini katika umuhimu wa Elimu bora ndani ya jamii zetu hapa
 Tanzania ,hivyo inaunga mkono Serikali ya Awamu ya  tano inayoongozwa 
na Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Mafuguli,alisema 
na kuongeza kuwa katika miradi mbali mbali ya elimu inayofanywa na benki
 hiyo lengo lake kuu ni kusaidia kuinua kiwango cha elimu na kuifikia 
kila jamii hasa maeneo ya vijijini .
"BankABC inatoa huduma ya Mkopo ambao ni mahususi kwa wafanyakazi wa serikali, Easy loans ambapo inakupa nafasi ya kulipa Mkopo kwa muda wa miaka sita na vile vile una uwezo wa kuweza kuongeza Mkopo hata kabla ya kumaliza kulipa ule wa awali,
Uzuri
 wa mkopo huu tofauti na mikopo mingine ni kwamba, mwenye kuomba Mkopo 
anaweza kuchagua ni mradi gani wa kuwekeza fedha zake kwa mfano kulipa 
karo ya shule, kununua gari, kufanya marekebisho ya nyumba, kulipa kodi 
ya nyumba au kumalizia ujenzi,Vile vile tunaweza kununua Mkopo wako wa awali ukabaki na Mkopo mpya",alisema Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi Bw. Emmanuel Nzutu  . 
Alisema
 Mkopo huo utakuwa na bima ya maisha pale ambapo mwenye Mkopo 
anapofariki, familia yake itapewa fedha  taslimu Tzs 500, 000 kwa ajili 
ya kugharamia mazishi.’ 
"Tunatoa
 wito kwa wateja wetu na wale ambao pia sio wateja wetu kujiunga na 
Bancabc na kuchangamkia Mkopo huu kwani sisi tunakuweka karibu na ndoto 
zako"alimaliza kusema Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi Bw. Emmanuel Nzutu .
Nae mkuu
 wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo,wakati akipokea msaada huo 
aliishukuru benki hiyo kwa msaada walioutoa wa kuchangia suala la elimu 
katika Wilaya yake,aidha pia DC Mtondoo  ameikaribisha benki hiyo kutoa 
huduma zao mbalimbali kwa Wananchi.
"BancABC tunawashukuru mno kwa msaada wenu mlioutoa,lakin pia tunawakaribisha msogeze pia huduma zenu kwa Wananchi wilayani hapa,ili Wananchi wanedelee kunufaika na huduma zenu mnazozitoa",alisema DC Mtondoo.

Mwakilishi wa benki ABC Bw. Emmanuel Nzutu
(Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akikabidhi msaada wa mabati kwa mkuu wa
wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo
Mwakilishi
wa benki ABC Bw. Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akiwa pamoja
na Asmah Abubakar(kushoto) kutoka kitengo cha masoko wa BancABC wakikabidhi
msaada wa mabati kwa mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo (kulia) 

.
Mheshimiwa Sauda Salum Mtondoo, mkuu wa Wilaya ya Kilindi akikabidhi mabati
yaliyotolewa na BancAbc kwa walimu wa shule ambazo zimenufaika na msaada huo.

Mwakilishi
wa benki ABC Bw. Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akiwa pamoja
na Asmah Abubakar kutoka kitengo cha masoko wa BancABC wakikabidhi msaada wa
mabati kwa mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo
 
No comments:
Post a Comment